Header Ads Widget

VIPIMO VYA DNA KUPATIKANA KILA KANDA KUMESAIDIA ONGEZEKO LA WAHITAJI NCHINI

Mkemia daraja la pili kutoka Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Ruben Sendelema

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Ili kupunguza changamoto za akina baba kuwakataa watoto na kumwachia mama pekee  na kusababisha adha kwa mtoto na mama,ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali kanda ya nyanda za juu kusini imewataka wanawake kutohofia gharama za kupima  vinasaba[DNA]Ili kubaini baba halisi.


Kauli hiyo imetolewa na Fundi sanifu mwandamizi kutoka mamlaka  ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA Kanda ya nyanda za juu kusini Rashidi Mjema wakati akizungumza na wanahabari mkoani Njombe katika maonesho ya viwanda vidogo SIDO yanayofanyika kitaifa mkoani hapa na kwamba gharama za kupima DNA ni shilingi laki tatu[300000] pekee jambo linaloweza kusaidia baba kulea watoto wake baada ya kupata ukweli.


Aidha amesema  uhitaji wa kupima vinasaba DNA ni mkubwa kutokana na udanganyifu uliopo katika mahusiano kwani baadhi ya akina baba wanawakataa watoto na kuwatelekeza wakimtupia lawama mama kuwa na mahusiano mengine.


Sanjari na hilo lakini pia Mjema amesema baadhi ya akina baba ambao   wanakataa majukumu yao   ni wengi kwa hiyo uhitaji huo ni mkubwa kwani katika kipindi cha mwezi mmoja katika ofisi za kanda zilizopo jijini Mbeya hufika watu 10 hadi 15 kutaka kupima vinasaba.


Hata hivyo amesema jeshi la polisi limekuwa likipata msaada mkubwa kutokana na teknolojia ambayo inabaini wahalifu katika matukio mbalimbali ikiwemo ujambazi.


Kwa upande wake Mkemia daraja la pili kutoka Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Ruben Sendelema amefafanua madhara ya sumu kuvu  ambayo  inapatikana kutoka na Fangasi ambao  wanaathiri  mazao kama mahindi,mchele na karanga.


Baadhi ya wananchi akiwemo Bi.Fortina Kahimba wamepongeza jitihada za serikali kutoa huduma ya upimaji DNA kila kanda kwani changamoto ya watoto kukataliwa na Baba imekuwa kubwa katika jamii na kusababisha Mama na watoto kuishi katika mazingira magumu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI