Header Ads Widget

VIJANA FANYENI KAZI ACHENI UNYWAJI WA POMBE ULIOPITILIZA" DC,MAKILAGI.

 


NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi amewaonya vijana wa Kata ya Pamba, kutoendekeza unywaji wa Pombe uliopindukia muda wa kazi hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi na  kujiingizia kipato.


Onyo hilo amelitoa leo wakati wa Usikilizaji wa Kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kupita Mtaa kwa Mtaa ili  kusikiliza kero.


Makilagi ameeleza kuwa unywaji wa pombe uliopitiliza Kwa vijana inasababisha kuwarudiaha nyuma kimaendeleo na kusababisha kuwa tegemezi Kwa wazazi wao na kuipoteza nguvu kazi ya Taifa Kwa ujumla.


"Vijana wa Kata hii mnaendekeza unywaji wa Pombe masaa ya kazi na ndiyo maana inakuwa vigumu kwa miladi ya Serikali inayotekelezwa Katika Kata zenu kuwaamini na kuwapatia kazi ya vibarua," amesema Makilagi



Hata hivyo amewataka wananchi wa kata hiyo kutoa taarifa za uvunjifu wa amani kwa kuripoti waalifu Katika mitaa yao ili kuvisaidia vyombo vya ulinzi na usalama kazi ya kuwakamata na kuwapeleka eneo husika.

Katika hatua nyingine Makilagi ametoa wiki Moja kwa maafisa Usafirishaji maarufu (Bodaboda) kuacha tabia ya kufunga mingirumo isiyokawaida kwenye pikipiki zao na kusababisha kero kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI