![]() |
Mosi Boniphace Ndozero; Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, katikati aliyeshika kibao akitoa maelekezo |
Na Mwandishi wetu, Iringa.
Ajali barabarani zimekithiri nchini
hasa kwa Watoto wadogo wanafunzi wa shule za msingi, ili kudhibiti ajali hizo
jeshi la polisi nchini kupitia kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa
limekuja na mbinu mpya ambapo limeanzisha klabu za usalama barabarani shuleni.
Akizindua kampeni hiyo Mratibu
mwandamizi wa jeshi la Polisi, Mosi Boniphace Ndozero amesema lengo ni
kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule za msingi waendelee kukua na utamaduni wa
usalama barabarani, na kujua namna bora ya kutumia mfumo wa barabara kwa maana
ya kuweza kuvushana watokapo nyumbani kuelekea shuleni na shuleni kuelekea
nyumbani.
“Hii ipo makusudi kabisa ili
kuwasaidia wanafunzi wasipate madhara pindi wanapotumia barabara, kwa mfano
ajali ambazo zinazima ndoto zao” alisema.
Kampeni ya hiyo imeanzia katika shule
nne ambazo ni, Tumain shule ya msingi, Ngome shule ya msingi, Maendeleo shule ya msingi
pamoja na Mlangali shule ya msingi zilizopo ndani ya manispaa ya Iringa, ambapo
jeshi la polisi limegawa vifaa maalumu (vinavyoitwa scholar patrol au junior
patrol system) watakavyotumia wanafunzi hao wakati wa zoezi hilo la
kuvushana barabara. “Kwa hiyo huu mfumo wanatumia vibao kama hivi, ambavyo
tumewaelimisha kwamba wanaposimamisha magari watakuwa wanaonesha kwenye alama
nyekundu watavuka na baadae watageuza upande wa kijani kuruhusu magari
kuendelea na safari” amesema Ndozero.
![]() |
Happiness Shayo; Mwalimu mkuu wa shule ya Msingu Tumain, akiongea na waandishi wa habari |
Akishukuru kwa mafunzo hayo kwa Watoto,
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tumain, Happiness Shayo, amesema, “sisi binafsi
itatusaidia kwa sababu watoto hawa ni wadogo wanahitaji kupewa uzoefu ni kwa
namna gani wanaweza kuvuka barabara kwa usalama.”
Mwisho
0 Comments