Header Ads Widget

TRA YAJA NA KAMPENI YA TUWAJIBIKE

 





Na Mwandishi wetu, Mtwara


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Mtwara imekuja na kampeni mpya ya ‘TUWAJIBIKE’ ili kuwezesha serikali kupata mapato yake bila udanganyifu wowote kwakuhamasisha utoaji wa risiti kwa wafanya bishara na kuwakumbusha wananchi kudai risiti ya bidhaa wanazonunua.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘TUWAJIBIKE’ Meneja wa TRA Mkoa wa Mtwara Elirehema Kimambo inayolenga kutoa elimu ya umuhimu wa utoaji wa risiti kwa wafanyabiashara pamoja na wanunuzi kudai risiti alisema kuwa wapo wafanyabishara sio wa kweli wamekuwa wakiandika bei pungufu na walichouza.


“Unajua kampeni hii ina malengo makuu mawili mojawapo likiwa ni kuwahimiza wauzaji kutoa risiti halali kwa mauzo yote yanayofanyika na kuwezesha wateja kudai risiti ya bidhaa waliozonunua ambazo zinatakiwa kuwa na TIN namba, anuani, tarehe na muda halisi ambao mauzo yamefanyika na kuwpeo na bei halisi ili kuondokana na ile tabia ya wafanyabishara kuandika 50000 kwa bidhaa iliyonunuliwa kwa shilingi laki mbili” alisema Kimambo


“Hata utoaji wa risiti halali bado haujakomaa katika jamii yetu hasa kwa mkoa wa Mtwara ambapo tumekuwa tukihimiza matumizi ya risiti halali za kieletronics ndio maana tumekuja na kampeni maalum ya tuwajibike ambapo tutashirkiana na wadau mbalimbali ili kuahamasisha wafanyabishara kutoa risiti na wananchi kudai risiti tutapita duka hadi duka na kuwakumbusha” alisema Kimambo



Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas alisema kuwa kuwepo kwa mazingira wezeshi kutaongeza uwezeshaji ndani ya mkoa wetu kwakuwa umepakana na nchi ambazo zinaweza kuwekeza katika nchi yetu kwakutumia njia za barabara, anga na maji.


“Nawasisitiza muwe marafkiki ili mtu akiuza atoe na akiuziwa aombe jambo la elimu kwanza ni muhimu na sio jambo la shuruti ni jambo la kisheria lakini linahitaji utayari na elimu isiwe na ukomo ili kila mmoja aweze kuona umuhimu huo namna mkoa wetu ulivyokaa unahamamsiha bishara za kimataifa kufanyika hapa lazima tuwavutie watu waweze kuja kufaya uwekekezaji ndani ya mkoa wetu” alisema Kanal Abbas



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI