Na,Jusline Marco Matukio Daima App Arusha
Wakazi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kujiandaa na uwepo wa mvua kubwa za El -nino katika mkoa huo zinazotarajiwa kunyesha kwa mujibu wa taatifa kutoka katika Mamlaka ya hali ya hewa TMA.
Tahadhari hii ni kutokana na Utabiri wa hali ya hewa uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kwamba, kuna uwezekano wa kupata mvua za juu ya wastani na awepo wa El - nino kwa baadhi ya mikoa kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba 2024 hadi Januari 2024 mkoa wa Arusha ukiwemo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella akizungumza jijini Arusha,ameziagiza taasisi zinazosimamia miundombinu mkoani Arusha kupita kwenye maeneo hatarishi ili kuyatambua na kujipanga kwa rasilimali zilizopo ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kutokea kutokana na mvua hizo.
Aidha amewataka viongozi wa ngazi zote kutoa elimu ya tahadhari kwa wananchi wote ili kuwa na ufahamu wa uwepo wa mvua hizo kubwa sambamba na kuwataka kuchukua tahadhari kabla ya hatari.
"Niwatake wananchi wote kujiandaa na kuchukua tahadhari ya mvua hizo, wale waishio mabondeni kuhama mara moja ili kujikinga na madhara yanayoweza kutokana na mvua hizo" ameweka wazi Mhe. Mongella.
0 Comments