Narcis Choma Meneja wa TANROADS mkoa Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAKALA wa barabara (TANROADS) mkoa Kigoma imeiomba bodi ya mfuko wa barabara nchini isaidie wakala huo kupata kiasi cha shilingi bilioni 35.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi maalum ikiwemo kufungua barabara ya Chankere hadi Mwamgongo kutokana na umuhimu wa barabara hiyo.
Meneja wa TANROADS mkoa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma alitoa maombi hayo akitoa taarifa ya utendaji kazi ya wakala huo kwa wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara waliokuwa wanafanya ziara kutembelea miradi iliyo chini ya bodi hiyo mkoani Kigoma.
Choma alisema kuwa katika fedha anazoomba zimo pia kiasi cha shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo makubwa barabara ya Kigoma hadi Kidahwe yenye urefu wa kilometa 28 ambayo muda wake wa kutumika umeisha na kwa sasa imekuwa na uharibifu mkubwa.
Sambamba na hiyo ameomba shilingi bilioni moja kujenga eneo la kuegeshea malori kwenye mizani ya Kazegunga,ujenzi wa barabara za njia mbili Kigoma hadi Mwandiga kilometa sita kwa shilingi bilioni tatu na ujenzi wa kizuizi kwenye njia ya treni kitakachogharimu shilingi milioni 800.
Akizungumza baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya barabara mkoani Kigoma Makamu Mwenyekiti Taifa wa bodi ya mfuko wa barabara, Octavian Mshiu alisema kuwa TANROADS imefanya kazi katika kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara na madaraja mkoani Kigoma na kuufuanya mkoa huo kwa sasa kufikika kirahisi kwa gari.
ambayo inaonekana kuleta faida na maendeleo ya kiuchumi kwa mkoa huo na watu wake.
0 Comments