Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa
Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Mhe.Deo Mwanyika
xxxxxxxxxxx
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Jumla ya vitabu 8000 vya ziada vimekabidhiwa kwa shule 17 za sekondari za serikali na 3 binafsi zilizopo Halmashauri ya mji wa Njombe kwa ajili ya kusaidia kupanua uelewa kwa wanafunzi.
Akikabidhi vitabu hivyo kwenye shule mbalimbali Mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika amesema anaamini vitabu hivyo vitakwenda kupunua ubongo kwa wanafunzi na hata walimu wenyewe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema jimbo la Njombe mjini limepata mbunge mwenye uwezo mkubwa wa kupandisha kiwango cha elimu tofauti na sasa.
Mgeni wa heshima katika zoezi hilo ni mkuu wa Wilaya ya Njombe ambaye amesema hataki kusikia vitabu hivyo vinauzwa ua kupelekwa katika maeneo yasiyotarajiwa hivyo vikawe msaada katika elimu kwa watoto wa halmashauri ya mji wa Njombe
Baadhi ya wanafunzi toka mabatini sekondari kwa niaba ya Shule nyingine Gerwin Kivi na Debora Kilasi wameahidi kwenda Kuubadilisha mkoa wa Njombe kwa masomo ya Sayansi
Akizungumza na kwa niaba ya wakuu wa shule Mwalimu Jimmy Ngumbuke amesema Baada ya Mbunge akitoa vitabu hivyo wao wanakwenda kuwanoa watoto Huku akiwaomba madiwani kwenda kuwahamasisha wazazi Juu ya watoto kupenda elimu.
Kwa niaba ya wazazi na wananchi mjini Njombe bwana Florence Bujeni amesema Urithi pekee wa mtoto ni elimu hivyo anaamini Mtoto akipata elimu Bora ataepukana na migogoro iliyopo katika jamii.
Mwakilishi wa Idara ya elimu sekondari Halmashauri ya mji wa Njombe Augusta Wella ameahidi kuvitumia vitabu hivyo kwa usahihi mkubwa na kuvitunza ili vije kuwasaidia wanafunzi wengi zaidi.
0 Comments