Header Ads Widget

TAMASHA KUBWA LA FASIHI KUFANYIKA ZANZIBAR



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR 

Jumuiya ya fasihi Zanzibar imeandaa tamasha kubwa la fasihi simulizi Zanzibar ambali linatarajiwa kuanza octobar 20 hadi 22 mwaka huu  katika ukumbi wa Idrisa Abdul wakili huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais  wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt Hussein  Ali Mwinyi.


Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika Ukumbi  wa Jumuiya ya Walemavu Zanzibar  UWZ Mhadhiri wa chuo Huria Tawi la Zanzibar Salma Omar Hamad amesema kwamba, lengo la Tamasha hilo ni kujenga hamasa  ya kuandika vitabu kwa Waandishi chupikizi kuandika vitabu na kuitangaza Zanzibar.


"Tamasha hili litachochea Uandishi wa Vitabu vya Fasihi ambavyo vitatumika kutangaza Utalii wa Zanzibar," amesema.


Amesema, Tamasha hilo pua lina lengo la kujenga  hamasa kwa Wananchi kupenda  kusoma  kazi za fasihi na kujifunza  mambo  mbalimbali.


"Tamasha  hili litainua ari kwa Waandishi wa Vitabu  pamoja na Wananchi kujifunza vitu mbalimbali  kupitia wageni  watakao  hudhuria katika Tamasha hilo," ameeleza.


"Ukweli kwamba Asilimia kubwa ya Wananchi  Visiwani  hawana mazoea  ya kusoma Vitabu kupitia Tamasha hili tutajenga  ari ya kupenda kusoma  vitabu  na kujifunza  mambo  mbalimbali," ameongeza.


Hata hivyo ameeleza  kuwa Tamasha  hilo linatarajia  kuhudhuriwa na Waandishi  mbalimbali  wa vitabu  kutoka  Ndani  na Nnje ya Zanzibar.


"Hata hivyo  Mwandishi  mkongwe  na Mshindi wa Tunzo  ya Nobel  anatarajiwa kuwepo  katika  Tamasha hilo," Amefafanua.


Nae Mwandishi Mkongwe  wa Vitabu  vya Fasihi na Mwandishi mwandamizi  wa Habari Ali Saleh amesema kuwa katika Siku za Tamasha  kutakuwa na uzinduzi  wa vitabu cha Zubeda kachoka ambacho kimebeba Hadithi 13 ndani  yake.


Amefahamisha kwamba, Katika Safari yake ya Uandishi wa Vitabu vya Fasihi ameandika  vitabu vilivyobeba Maudhui mbalimbali  kwa maslahi  ya taifa.


Kwa upande wake, Mhandhiri Kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  SUZA Dkt. Mariam Jaffar Ismail amesema kwamba, katika tamasha  hilo kutakuwa na shughuli mbalimbali kama vile Usiku wa Mashairi.


"Kutakuwa  na Usiku  wa Mashairi, Kazi za Watoto pamoja na siku malumu ambayo kutawasilishwa Umuhimu wa Matumizi  ya Kiswahili, " ameeleza.


Tamasha hilo limeandaliwa na jumuiya ya fasihi Zanzibar kwa kushirikiana na wizara ya utalii na mambo ya kale ambapo kauli mbiu ikiwa ni Fasihi ya Zanzibar ulimwengu ndani ya Maneno.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI