NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMA APP MWANZA.
Serikali imesema itahakikisha inatumia takwimu za wanawake ili kusukuma maendeleo mbele ikiwa ni pamoja kuendeleza mashirika mbalimbali Kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ya Asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri husika.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi alipokuwa akifungua Kongamano la wanawake lililiwakutanisha zaidi ya wanawake 250 kutoka Mikoa mbalimbali hapa Nchini yenye lengo la kuwajengea uelewa kwenye masuala ya uongozi na afya ya akili.
Makilagi amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya ushirika Kwa ujumla
katika kuendeleza wanawake kwa kuwapitia mitaji kupitia mikopo na kuwajengea utaratibu mzuri wa kuweka akiba zao kwa matumizi ya baadae.
"Sote tunafahamu dhamira ya Serikali ya Awamu ya sita katika kuwainua wanawake kiuchumi kupitia mikopo midogo midogo na mikubwa kuwaongezea fursa zaidi katika nafasi za uongozi katika nyadhifa za juu" Alisema Makilagi
Amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya ushirika Kwa ujumla katika kuwaemdeleza wanawake Kwa Kwa kupitia mitaji kupitia mikopo ya ushirika katika kuendeleza wanawake.
Somoe Nguhwe; Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake vyama vya ushirika Tanzania
Mfumo dume kwa baadhi ya mikoa inayomnyima mwanamke nafasi ya kuchangamkia fursa za kiuongozi katika vyama na ngazi za juu kwa mujibu wa mfumo wa uongozi wa vyama vya Ushirika Kutokana na kutojiamini kwa baadhi ya wanawake juu ya uwezo walionao katika kuongoza vyama.
"Kumekuwa na baadhi ya wanawake kujitenga na mitandao ya wanawake inayoweza kuwajengea uwezo wa kupiga hatua zaidi kimaisha hiyo nayo inaweza kusababisha wanawake kurudi nyuma" Alisema Somoe.
Nae mratibu wa Jukwaa Hilo la wanawake Leah Daud amesema pamoja na mambo mengine wanawake watapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya uongozi na namna ya kuepuka mikopo umiza.
0 Comments