Header Ads Widget

PWANI YATAKA WAWEKEZAJI WATUMIE MAENEO YALIYOTENGWA KWA UWEKEZAJI

 


MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka wawekezaji kutumia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ambayo yamewekwa miundombinu muhimu pia kuepuka kutapeliwa.


Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alipotembelea kiwanda cha King Lion Investment (King Lion Steel Mill) kinachojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za chuma kilichopo eneo la viwanda la Zegereni Wilayani Kibaha.


Kunenge amesema kuwa serikali inatekeleza miradi mbalimbali kwenye maeneo ya uwekezaji ikiwemo ya Barabara, Umeme, Maji na Gesi ili kuvutia uwekezaji ambapo ni tofauti na maeneo ambayo si rasmi kwa uwekezaji huwa na changamoto kupeleka miundombinu.


Kwa upande wake meneja wa kampuni hiyo Arnold Lyimo amesema kuwa mradi huo unagharama ya zaidi ya shilingi bilioni 160 na kitakuwa kiwanda kikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na utakamilika Juni 2024 na kuanza uzalishaji.


Lyimo amesema kuwa kitakapokamilika kitazalisha chuma tani 350,000 kwa mwaka ambapo malighafi za kuzalishia chuma na zitauzwa ndani na nje ya nchi zikiwemo Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo na  kitatoa ajira 400 za moja kwa moja na 5,000 zisizo za moja kwa moja

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI