Header Ads Widget

GLOBAL LINK YAJA KIVINGINE, YAAHIDI MAKUBWA KWA WATEJA WAKE

 





Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar


Taasisi ya Global link imewataka wadau wake kuisemea vizuri na kuikosoa  taasisi hiyo ili iweze kufanya vizuri katika kuwahudumia wadau mbalimbali wanaotaka huduma ya  kusoma nje ya nchii ili waweze kupiga hatua ya pamoja.


Rai hiyo ametolewa jijini Dar es Salaam na Mkurigenzi wa Taasisi hiyo, Abdulmalik Mollel, wakati alipokua katika kilele cha maadhimisho cha wiki ya huduma kwa mteja ambapo amesema kufungwa kwa kilele hicho ni mwanzo mpya wa kutoa huduma zenye ubora kwa mwaka 2024 ambapo imejipanga vizuri ili kuhakikisha inafanya vizuri kimataifa.


Amesema kuwa, kuikosoa taasisi hiyo katika utendaji kazi wake ikiwemo huduma wanazozitoa kwa wadau mbalimbali, wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma nje, inaonesha ni kwa namna gani ambavyo wadau wanaifatilia kwa ukaribu tena kwa nia njema hivyo watachukulia changamoto hiyo kama njia bora kutatua mapungufu yalipjitokeza.


"Kupokea maoni na ushauri hata kukosolewa, kwetu tunachukulia ni njia ya kutatua changamoto kwa wateja wetu, kwani kuskiliza maoni na ushauri  imetusaidia kufanya vizuri  kwa miaka 16 tangu kuanzishwa kwa taasisi hii, katika kutoa huduma zetu kwa wadau wetu, tunaahidi kila changamoto aliyonayo mteja wetu ndio mtaji wa huduma na tutamfanyia aridhike kuendelea kupokea huduma kutoka kwetu"amesema Mollel.


Ameongeza kuwa, kuanzia mwaka 2024 wadau wao wategemee mambo mazuri kutoka taasisi hiyo, ikiwemo kufungua dirisha la usajili kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma nje kuanzia mwezi Januari hadi Disemba sambamba na kupokea wanafunzi wakigeni kutoka mataifa mbalimbali kuenda kusoma Tanzania jambo ambalo litafungua fursa mpya kwa vijana wa kitanzania.


Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtemdaji wa Kampuni ya Ndalini Media, Anna Massawe amesema kuwa kitu pekee kilichomfanya aipende taasisi hiyo ni kutokana na namna bora inavyotoa huduma kwa wateja wake.


"Mimi sisemi ada ni ndogo au kubwa bali huduma wanayotoa ni bora kabisa, unampeleka mtoto wako kwenda nje ya nchi kusoma wanafatilia hadi maendeleo yake katika masomo na sio kumuachia jukumu hilo mzazi peke yake hii imenifanya niipende sana hii taasisi na nimeshawaunganisha marafiki zangu wengi na wao wamefurahia huduma yao"amesema Anna.


Akizungumza katika hafla hiyo, Beatrice Senea ambae ni miongoni mwa wazazi waliopeleka watoto wao nje ya nchi, amesema, mzazi anapotaka kumpeleka mtoto wake kusoma nje ya nchi asiangalie gharama bali huduma anahopatiwa kwa mtoto wake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI