Header Ads Widget

MGOMBEA WA UWAKILISHI JIMBO LA MTAMBWE PEMBA AENGULIWA KWA UDANGANYIFU

 




Na THABIT MADAI, ZANZIBAR 


Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemuengua Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Mtambwe, Mkoa- Kaskazini Pemba Mohammed Ali Suleiman (ACT WAZALENDO) Kwa kile kinachodaiwa udanganyifu wa Kitambukisho la Mzanzibar Mkaazi.


 ZEC kisiwani Pemba imethibitisha hilo na kusema kuwa Mgombea huyo aliwekewa pingamizi Kwa Madai ya kuwa na vitambulisho viwili vya Mzanzibari Mkaazi vinavyosomeka Kwa nambari mbili tofauti jambo ambalo ni kosa kisheria.


Mgombea  Ali Suleiman anadaiwa kufanya udanganyifu wa kutoandika nambari sahihi inayopaswa kutumika katika fomu yake na kufanya Mgombea huyo kupoteza sifa.


Katibu wa Idara ya Habari na Uenezi wa Chama cha Act Wazalendo  Salum Biman amesema kuwa  hadi sasa bado taarifa rasmi ya kuenguliwa kwa Mgombea wa Chama hicho bado hawajaipokea kutoka Tume ya Uchaguzi  licha ya kuona taarifa kwenye  mitandao ya  kijamii na baadhi ya Vyombo  vya habari.


"Tumezisikia Taarifa ila bado hatujapokea Taarifa rasmi kutoka ZEC juu ya kuenguliwa kutembea Uwakilishi kwa Mgombea wetu katika jimbo la Mtabwe Pemba," Amesema Bimani.


Jimbo la Mtambwe linafanya Uchaguzi mdogo Baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Habib Mohammed Ali  ACT WAZALENDO kufariki Dunia mwanzoni kwa mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI