Na THABIT MADAI,ZANZIBAR
MBUNGE wa Viti maalumu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kundi la watu wenye ulemavu, Stella Ikupa amepeleka tabasamu kwa Watu wenye ulemavu Visiwani Zanzibar kwa kutoa Msaada wa Miwani,Kofia,Mafuta, Bakora nyeupe, Magongo ya kutembelea pamoja na Viti vya Magurudumu.
Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milion Saba ambao una lengo la kuwaunga Mkono watu wenye ulemavu katika kisiwa Cha Unguja.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Msaada huo Mbunge ambae pia mwanzilishi wa taasisi ya Ikupa Trust Fund, Stella Ikupa amesema kwamba uwamuzi wa kutoa Msaada huo ni kuendelea kuwaunga mkono watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwapungizia changamoto zinazowakabili.
Amesema, msaada huo utawasaidia watu wenye mahitaji maalumu katika kukabiliana na baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili katika maisha yao ya kila siku
"Nimetoa toa msaada huu katika kuwaunga mono ndugu zangu wenye mahitaji maalumu katika kisiwa cha Unguja lengo likiwa kushika mkono na kuwaondolea baadhi ya changamoto katika maisha yao ya kila siku," amesema.
Aidha amefahamisha kuwa msaada kama huo anatarajiwa kuutoa katika kisiwa cha Pemba kwa makundi mbslimbali ya Watu wenye Ulemavu.
"Katika kuunga Mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais Dkt Mwinyi tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa misaada mbalimbali kwa zetu wenye mahitaji maalumu ili kuwapungizia changamoto ambazo zinawakabili," Ameeleza.
katika hatua nyingine Mbunge huyo ametoa wito mbalimbali kwa jamii kutoa watenga watu wenye ulemavu katika harakati mbalimbali za maisha ya kila siku.
"Naomba jamii iwaone watu wenye ulemavu ni kama watu wengine wasio na ulemavu. Kuwa na ulemavu siyo jambo la ajabu,Jamii ituone sisi watu wenye ulemavu wanaume au wanawake kama watu wengine ambapo haki kama watu wengine,"amesema.
Akipokea Msaada kwa niaba ya Watu wenye Ulemavu, Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Tunu Juma kondo amepongeza hatua ya Mbunge huyo kutoa msaada kwa watu wenye ulaemavu huku akitoa wito kwa Wabunge wengine kuiga mfano huo.
"Watu wenye ulamavu wanahaki kama watu wengine katika jamii hivyo tunaoaswa kujitokeza kwa wingi katika kuwasaidia kama alivyofanya Mbunge Stella Ikupa kwa kuwasaidia na kuwaunga Mkono," ameeleza.
Kwa upande Watu wenye ulemavu walimshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo na kuahidi vitumia kama msaada huo ulivyokusudiwa.
0 Comments