Header Ads Widget

MAKAMU WA RAIS AAGIZA HADI OCT 30 MWAKA HUU APATE TAARIFA ZA KINA ZA KUTOFUNGWA KWA MITAMBO KWA MIAKA MIWILI SASA KATIKA KIWANDA CHA DAWA MAKAMBAKO NJOMBE

Makamu wa Rais Dokta Philip Mpango akiwa katika kiwanda Cha dawa Idofi MAKAMBAKO Njombe leo
Naibu waziri wa afya Dokta Godwin Molel


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Philip Mpango ameagiza kabla ya octoba 30 mwaka huu kuwasilishwa kwa taarifa ya kwanini baadhi ya mitambo katika kiwanda Cha dawa Idofi Makambako Njombe haijafungwa kwa miaka miwili sasa.


Dokta Mpango ametoa agizo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho  na kupokea kero hiyo toka kwa mbunge wa jimbo la Makambako na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambaye amesema haiwezekani mitambo ya kuchakata bidhaa nyingine isifungwe kwa mwaka wa pili Sasa na kusababisha hoja kwa mkaguzi wa hesabu za serikali CAG.


Naibu waziri wa afya Dokta Godwin Molel amesema pamoja na hoja zilizoibuliwa na CAG na kuanza kufutwa kwa hoja hizo lakini bado uzalishaji wa mipira ya mikono na Dawa utaendelea kufanyika Idofi na tayari waziri ameelekeza zitengwe bilioni 2 kwa ajili ya kufunga mitambo.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema  mchakato wa miradi mingi  ya serikali  umekuwa na Changamoto nyingi ilihali mtu binafsi akiamua kuwekeza mradi huo huo anafanya vizuri na ndio sababu zinazosababisha hata kiwanda Cha Dawa Cha Idofi kuwa na hoja za CAG.


Malalamiko hayo yamemfanya Makamu wa Rais Dokta Mpango kutoa maagizo hayo na kuagiza watumishi wa MSD kuhakikiwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi yao kuhujumu viwanda.

Nao Wananchi wa Makambako akiwemo Jeremiah Kinyunyu Florenciana Msiami na Charles Mtifu  wamesema changamoto ya upatikanaji wa dawa inapaswa kutatuliwa kwa kujengwa viwanda kama Cha Idofi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI