Header Ads Widget

MADIWANI KIGOMA UJIJI WATAKIWA KUSHUGHULIKIA KERO ZA WANANCHI

Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji Mwantumu Mgonja akizungumza kwenye kikao cha baraza

Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa kwenye kikao cha baraza
 

Katibu Tawala wa wilaya Kigoma Mganwa Nzota (kushoto) akitoa salamu kwenye kikao cha baraza la madiwaji la Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MADIWANI katika halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kutumia muda wao mwingi kuwa kwenye kata zao kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi na kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wao.


Katibu Tawala wa wilaya Kigoma Mganwa Nzota alisema hayo akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji lililokuwa likipokea taarifa za utendaji za kata kwa kipindi cha miezi mitatuh iliyopita na kusema kuwa ofisi za kata kwa madiwani wakishirikiana na watendaji wa kata wanayo nafasi kubwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Kigoma,Salum Kali alisema kuwa ofisi ya Mkuu wa wilaya imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wananchi wenye kero, malalamiko na changamoto ambazo zinaweza kufanyiwa kazi kwenye ngazi za kata hivyo madiwani na watendaji wakitimiza wajibu wao hilo linawezekana.


Akieleza kero za kata yake  katika kikao hicho  diwani wa kata ya Buhanda, Kilahumba Rutuli ameomba halmashauri kuona uwekezekano wa kujengwa kwa shule mpya ya msingi kutokana na shule iliyopo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambapo kwa sasa ina wanafunzi 2500.


Naye Diwani wa viti Maalum kata ya Gungu, Zabibu Mtende ameiomba halmashauri kuona uwekezekano wa kujengwa haraka kwa zahanati kwenye kata ya Gungu mtaa wa ujenzi kutokana na eneo hilo kutokuwa na kituo chochote cha huduma ya afya kwani ujenzi umeanza kwa kujengwa msingi ambao kwa muda mrefu sasa umeshindwa kuendelezwa.


Akizungumza kabla kuhitimishwa kwa kikao hicho cha baraza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma, Mwantumu Mgonja alisema kuwa halmashauri inakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa fedha na kwqmba 

Kutokana na hilo Mgonja alisema kuwa wanajua uwepo wa miradi mingi iliyoanza (miradi viporo) ambayo haijakamilika na kwamba kupitia mapato ya ndani watafanya kazi kubwa kuhakikisha miradi mingi inatekelezwa na  kumalizika ili iweze kutumika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI