NA MAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kamati ya kudumu ya bunge ua uwekezaji wa mitaji ya umma imeitaka serikali kuwekeza kwenye wataalamu wa mionzi(Nyuklia)katika tume ya nguvu za Atomu Tanzania(TAEC) ili uwekezaji waliofanya wa kutanua ofisi maeneo mbalimbali pamoja na ujenzi wa maabara kubwa uweze kuleta tija.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo Augustine Vuma Holle wakati walipotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya tume hiyo mkoani Arusha ambapo alisema kuwa wameona kuna upungufu wa wataalamu wa mionzi hivyo wametoa rai kwa serikali kuwekeza katika eneo hilo kwani katika tume hiyo kuna wataalamu wa mionzi sita na wanategemewa nchi nzima na katika sekta zote.
“Tumeona kwa miaka mitatu iliyopita ofisi zimepanuka, zimekuwa nyingi karibia asilimia 400 ambapo zimeongezwa ofisi 58 wakati awali zilikuwa ofisi 12 na ni maendeleo makubwa sana kwahiyo serikali inavyoendelea kupanua miundombinu hii ya majengo na maabara hizi lazima pia iendelee kuendeleza wataalamu wa mionzi,”Alisema Mbunge Holle.
“Serikali watenge fedha za kutosha na kuwa na mpango mkakati mzunzi wa kuhakikisha wataalamu wanaongezeka na kuwa wengi ili uwekezaji kwenye majengo haya tija yake iweze kupatikana lakinj pia tunaipongeza serikali kwa kazi nzuri ya uwekezaji huu kwani ni mzuri na wa kiwango cha juu,” Alieleza.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa idara ya sayansi, teknolojia , ubunifu kutoka wizara ya Elimu sayansi na teknolojia Prof. Ladslaus Mnyone alisema kuwa Tume hiyo ina majukumu mbalimbali mojawapo ikiwa ni kufanya tafiti na ubunifu kwenye eneo la teknolojia ya mionzi ambapo tekmolojia hiyo inamanufaa kwenye sekta karibia zote ikiwemo Afya na Kilimo.
“Tume hii ina jukumu la kuthibiti matumizi ya mionzi kwasababu mionzi isipotumika vizuri inaweza kusababisha athari kwahiyo lengo hasa ni kuhakikisha yeknolojia hii inatumika kuleta manufaa kwa kuwasaifia watanzania katika sekta mbalimbali bila kuwasababishia athari,”Alisema Prof Mnyone.
Alifafanua kuwa fursa za teknolojia hiyo bado ni nyingi ndani ya nchi na nje ya nchi hivyo watahakikisha maabara hiyo inatumika kuzqlisha matokeo ya tafiti na kujibu changamoto kwenye teknolojia husika ikiwa ni pamoja na kuongeza firsa za matumizi ya teknolojia hiyo.
“Kama mnavyofahamu katika nchi nyingine mfano China teknolojia ya nyuklia inatumika katika kuzalisha umeme kwahi hili limaweza likawa ni eneo mojawapo ambalo wataalamu wetu wanaweza kulifanyia utafiti na kuona namna ya kutumia lakinibpia teknolojia hii inaweza kutumika kuangamiza biumbe waharibifu wanaoweza kuleta athari mfano Mbung'o,”Alisema.
Aliendelea kusema kuwa miundombinu hiyo itumike kuzalisha rasilimali watu kwani msingi wa tafiti na ubunifu ma huduma nyingine zote ni rasilimali watu wenye weledi stahiki hivyo wanategemea kwasababu ya tume hiyo ambayo ina miundombinu ya kisasa na vifaa vya kisasa kutakuwa na fursa ya kuwa na vijana wa kitanzania katika yeknolojia hiyo lakini pia tutatuwa kituo cha kutoa mafunzo ndani ya bara la Afrika na nje ya bara la Afrika.
Naye mkurugenzi mkuu wa TAEC Prof Lazaro Busagala alisema kuwa maabara hiyo yengamano imegharimu Bilioni 10.4 na limekamilika kwa asilimia 100 ambapo lilianza kujengwa Septemba 2019 na kukamilika Septemba 2022.
Hata hivyo tume hiyo inahusika na hosipitali zote zinazotoa tiba kwa njia ya mionzi, makampuni ya ujenzi wa barabara, viwanda vinavyotumika kutengeneza mbegu chotara mazao mbalimbali kwaajili ya kutoa matengenezo ya vifaa vinavyotumia teknolojia ya Nyuklia.
0 Comments