NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi amewataka watendaji, na wenyeviti wa mtaa kutumia takwimu za sensa ya watu na makazi katika mipango yao ya kazi hatua itakayosaidia kufukisha huduma za kijamii ikiwemo umeme, maji na masoko.
Kauli hiyo ameitoa katika ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Kwa viongozi watendaji, wenye viti wa mitaa pamoja wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii yaliyofanyika katika chuo Cha ualimu butimba Mkoani hapa.
Makilagi amesema kuwa takwimu rasmi za sensa zikiwemo za watu ndio zinazotumika katika kufanya maamuzi yanayohusu sera na mipango ya maendeleo yatakayoleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kazi na kusaidia upatikanaji wa maendeleo katika Wilaya hiyo.
"Nchi zote na sio Tanzania pekee zinapotaka kufanya maendeleo ni lazima kutumia takwimu za sensa" Alisema Makilagi.
Kwa upande wake Meneja idara shughuli za takwimu Taifa Benedict Mgambi Amesema kuwa serikali iko katika utekelezaji wa awamu ya tatu na mwisho ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Serikali imekamilisha kuandaa na kuzidua ripoti kumi na moja za sensa ikiwa ni pamoja na ile ya mwanzo zikiwa zimejikita katika mgawanyo wa idadi ya watu Kwa maeneo ya kiutawala Hadi ngazi ya kata ikiwa imejikita katika mgawanyo wa idadi ya watu kwa umri na jinsia Hadi ngazi ya Halmashauri Kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
"matokeo yote ya sensa ambayo hadi sasa yamezinduliwa yamefanyiwa uchambuzi hadi ngazi sasa yamezinduliwa yamefanyiwa uchambuzi hadi ngazi ya kata ingawa lengo letu ni kufika ngazi ya chini ya utawala Yani vitongoji Kwa maeneo ya vijiji na Miata Kwa maeneo ya mjini" Alisema
Mgambi amesema kuwa matokeo ya awali ya sensa katika ngazi hizo yanatolewa Kwa matumizi maalumu Kwa wenye uhitaji wakati wa uandaaji ripoti husika.
"Tunafahamu kuwa wako WADAU wengi ambao wanahitaji matokeo ya sensa katika ngazi za chini za utawala Kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uandaaji na utekelezaji wa program za maendeleo"
0 Comments