Header Ads Widget

ZIPA YATANGAZA ENEO LA UWEKEZAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

 


NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR


KUFUATIA adhma ya Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi ya kuifungua Zanzibar kiuchumi, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imetangaza fursa za Uwekezaji wa Mafuta na Gesi Asilia katika Eneo la Mangapwani lenye Ukubwa wa Hekta 47.53.


Akitoa taarifa leo kwa Waandishi wa Habari ofisini kwake Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Mkurugenzi Mtedaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ZIPA, Sharif Ali Sharif amesema kuwa Serikali imetenga eneo la Mangapwani lenye ukubwa wa Hekta 47.53 kwa ajili ya Uwekezaji wa Mafuta na Gesi Asilia ambapo amewataka wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika Eneo hilo.


Amesema, hatua imekuja kufuatia adhma ya Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi  ya kuifungua Zanzibar kiuchumi na kuleta maendeleo kwa Kasi.


Mapema Mkurugenzi wa Utafiti wa Miradi ZIPA Emmanuel Mashimba ameeleza kuwa Masharti ya Uwekezaji katika eneo hilo lililotengwa kwa uwekezaji wa Mafuta na Gesi Asilia ni pamoja na kuweza kutunza mazingira.


Eneo la Mangapwani ni moja ya eneo la Kimkakati lililotengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Uwekezaji na ujenzi wa Bandari ya Mafuta na Gesi Asilia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI