Header Ads Widget

MPANGO WA KUTOA VYETI KWA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI WAANDALIWA

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WAKALA wa usajili ufilisi na udhamini (RITA) unatarajia kuzindua mpango wa uhamasishaji wa usajili wa Watoto chini ya miaka mitano ili waweze kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

 


Hayo yameelezwa katika semina ya siku moja kwa viongozi waandamizi wa serikali, viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya serikali lengo likiwa kukabiliana na changamoto ya jamii kushindwa kuwasajili watoto wao na kuwakatia vyeti vya kuzaliwa.


 Naibu Kabidhii Mkuu wa serikali RITA, Irene Lesulie alisema kuwa mpango huo unalenga kusajili na kutoa vyeti kwa Watoto wote chini ya miaka mitano waliozaliwa nchini na hiyo inatokana na idadi ndogo ya Watoto waliosajiliwa na kupata vyeti ukilinganisha na Watoto waliozaliwa.



Akitoa takwimu za idadi ya Watoto waliozaliwa na kupata vyeti Lesulie alisema kuwa kwa mwaka jana jumla ya Watoto 442,662 walizaliwa mkoani Kigoma ambapo kati yao ni Watoto 46,480 waliosajiliwa na kupata vyeti ikiwani asilimia 10 ya Watoto waliozaliwa.



Akizungumza wakati akifungua semina hiyo  Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa mpango huo utaleta manufaa makubwa kwa mkoa kuwa na idadi ya Watoto ambao watatoa taswira nzuri katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

 


Katika hotuba iliyototolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Buhigwe, Michael Ngayarina alisema kuwa Pamoja na umuhimu huo ametaka watendaji wa serikali wanaosimamia zoezi hilo kuhakikisha taratibu za upekuzi na utambuzi za watu wanaopaswa kupewa vyeti hivyo zinazingatiwa.



Kwa upande wake Mwakiklishi wa Mkurugenzi Msaidizi huduma za ustawi wa jamii TAMISEMI,Mariam Mkumbwa ametaka watendaji wanaosimamia zoezi hilo kuhakikisha taarifa zinazokusanywa kuingizwa kwenye mifumo ili Watoto wanaosajiliwa na kupewa vyeti waweze kusomeka kwenye mifumo mahali popote nchini.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI