Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Doto Biteko ameitaka Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushirikiana na taasisi zote za serikali, kuwa na Mfumo mmoja utakao weza kutoa taarifa za Kijiografia lengo ili kuweza kupima miji yote nchini na kumaliza migogoro iliyopo.
Hayo ameyasema leo Jijini Dodoma kwenye Hafla ya ufunguzi wa kituo Cha Taifa cha ubunifu na mafunzo ya Teknolojia ya taarifa za Kijiografia akimuakilisha Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa.
Amesema wizara ya ardhi ni Wizara mama ambapo karibu kila wizara zimekuwa zikiigusa wizara hivyo mashirikiano mazuri kwa wizara nyingine ndizo zitaweza kuandoa migogoro kwa kuhakikisha Maeneo yanapimwa yanapanga kurasimisha.
" Kumekuwepo na wimbo la migogoro isiyoeleweka na mtatuzi wake ni wizara na iko wazi panapotokea migogoro kunamtu katikati na mtatuzi Sasa niwaombe twendeni tukafanye kazi tuliosemea kwa weledi na tukifanya hivyo tutakuwa tumeondoa urasimu kwa Watanzania," Amesema Dkt Biteko
Aidha Amemuagiza Waziri wa Ardhi nyumbani na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa kukifanya kituo hicho cha Ubunifu ya Teknolojia ya taarifa za Kijiografia kugomewa na Watanzania kwa kuja kusoma na kujifunza badala ya kulipana Fedha za Mafunzo .
Pia akiwataka wahitimu waliopatiwa vyeti nawao kuwa walimu kwa kuwa chachu ya babadiliko kwenye upatikanaji wa Kijiografia huku akisisitiza Mafunzo hayo yawe endelevu hali itakayosaidia kumaliza migogoro ya aridhi.
Naye Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Jerry Silaa amesema Serikali ya Tanzania Kwa kushirikiana na Serikali ya Korea imechukua hatua za kukabiliana na changamoto za ardhi kwa kuanzisha kituo cha TNGC .
Amesema Wizara hiyo ina changamoto ya ukosefu wa teknolojia za kisasa katika upatikanaji wa taarifa za kijiografia na mifumo ya usimamizi wa ardhi na kupelekea kupungua kwa kasi ya upangaji , upimaji,uthamini na umilikishaji ardhi hivyo kituo hicho kinatarajiwa kumaliza kero zote.
"Serikali yetu imeweka historia leo ya kuweka alama mbili muhimu ambayo ni kuzindua kituo cha kitaifa Cha Ubunifu na mafunzo ya taarifa za kijiografia na kuwatunuku vyeti wahitimu 11 waliopata mafunzo ya kurusha ndege zisizo na rubani tatu ,ukusanyaji wa taarifa za kijiografia na uchakataji wa taarifa za kijiografia,"amesema
Silaa ametumia nafasi hiyo kuwataka Viongozi wa TNGC kujipanga na kuwa na maono ya kukiendeleza kituo ili kiwe Taasisi pekee ya Ubunifu na usimamizi wa taarifa za kijiografia nchini na kwamba Wizara itaendelea kutoa ushauri na kukilea kituo hicho .
"Serikali itaendelea kukiwezesha kituo ili kifikie malengo yake na kusaidia kutatua changamoto ya wataalam wenye weledi na ujuzi wa teknolojia ya kisasa ya usimamizi taarifa za kijiografia,"amesisitiza
Naye Balozi wa Korea Nchini Tanzania Kim Sun Pyo Amesema kuzinduliwa kwa kituo hicho ni manufaa kwa wananchi wa Dodoma kwani wataweza kunufaika hasa Katika Suala zima la upimaji wa ardhi ambao Sasa unakwenda kufanyika kwa ubora na kwabai nafuu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Mhandisi Anthony Sanga ameeleza kuwa kituo hicho kina lengo la kujengea uwezo watumishi na wadau kukidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa ya usimamizi wa taarifa za kijiografia nchini kwa kutoa mafunzo yenye ujuzi maalum.
Amesema TNGC ni fursa ya kuanzishwa kwa miundombinu ya kitaifa ya taarifa za kijiografia nchini na kwamba itasaidia kusambaza na kubadilishana taarifa Kwa manufaa ya watanzania.
0 Comments