Header Ads Widget

AMON, WANAOIBA MITA ZA UMEME KWA WATEJA WETU HATUA KALI ZINACHUKULIWA DHIDI YAO.

NA CHAUSIKU SAID, MATUKIODAIMAAPP, MWANZA.

Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Mwanza limewataka wateja wao wote kuwa makini na matapeli wanaokwenda kuwatembelea nyumbani na kujitambulisha kuwa ni maafisa wa shirika hilo na kukagua miundombinu hiyo kisha kiwaibia mita za umeme.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa kitengo huduma Kwa wateja Mkoani hapa Amon Michael na kueleza kuwa tatizo hilo wameligundua baada ya kupata kesi 18 na wateja wao wengine  kufika ofisini kuripoti.


Amon ameeleza kuwa wamefanya uchunguzi na kugundua kuwa watu wasio waaminifu ndio wanafanya vitendo hivyo  wengine kutumia mita ambazo sio za kwako kwani uuziwa na watu wanaojifanya kuwa maafisa wa Tanesco 

"Niwaombe wateja wetu waelewe sisi tanesco tunataratibu zetu za kufanya ukaguzi wa miundombinu kwanza ni lazima Afisa ajitambulishe na aoneshe kitambulisho chake na Kuna fomu atajaza na mteja atasaini ndipo atafanya ukaguzi katika mita hiyo" Alisema Amon.


Hata hivyo amefafanua kuwa watu hao wanaojitambulisha kama maafisa wa tanesco kama hawatatumia taratibu hizo zilizowekwa na shirika hilo wateja wao wanapaswa kupiga simu ya dharura ili kupata msaada wa haraka.


 Aidha amewataka watu wote wenye tabia hiyo kuachana nayo mara moja kwani huo ni uhalibifu wa miundombinu ya serikali.


Kwa upande mwingine amewataka wananchi kutokubali kudanganywa kutoa rushwa ya fedha ili kufikishiwa huduma ya haraka, kwani ili kupata huduma kutoka tanesco nilazima kumlipia banki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI