Header Ads Widget

WAZEE KIGOMA WAPEWA BIMA ZA AFYA.

 


Na Editha Karlo,Kigoma

TAASISI ya Endeleza Wazee Kigoma(EWAKI)imetoa bima za afya kwa wazee wazee 400 zenye thamani ya shilingi milioni 3 kwaajili ya wanufaika 2400 ambao ni wazee na wategemezi wao.


Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi bima hizo Kaimu katibu tawala Mkoa wa Kigoma Ntime Mwalyambi alisema jukumu la kutunza wazee lisiachwe mikononi kwa Serikali na Taasisi binafsi bali kila mtu awajibike kuwatunza wazee.


“Wazee ni tunu ya Taifa bila wao sidhani kama tungeweza kufika hapa tulipo leo,hivyo ni jukumu la kila mtu kuguswa na uwepo wao ili waendelee kufurahia maisha”alisema katibu Tawala


Naye Mwenyekiti wa mtandao wa mashirika ya wazee Tanzania ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa EWAKI Bi Clotilda Kokupima alisema kutokama na utafiti waliofanya wamegundua hitaji la matibabu kwa wazee ni changamoto inayoongoza kwa wazee wengi Mkoani Kigoma.


“Kwenye utafiti wetu huo tumeuliza vitu mbalimbali ikiwemo usalama,hitaji la chakula,mavazi,usafi na mengine ila tumeona afya kwani wazee wengi wanashindwa kumudu gharama za matibabu”alisema Kokupima.


Mkurugenzi wa EWAKI alisema mpango wa utoaji wa bima hizo kwa wazee ni endelevu kwa kipindi cha miaka miwili,ambapo mwaka 2024 matarajio yao ni kutoa bima kwa wazee 2400 ili kufikia lengo la kutoa bima 4800 walilojiwekea.


Upande wa Afisa maendeleo ya jamii ofisi ya Mkuu wa Mkoa Anna Akyoo aliishukuru taasisi hiyo na kutoa wito kwa taasisi nyingine za kiraia kusaidia changamoto mbalimbali za wazee.


Baadhi ya wazee walioshiriki hafla hiyo waliishukuru Taasisi ya EWAKI kwa kuwapatia bima za matibabu,pia waliiomba serikali pamoja na wadau wengine kutokuwasahau kwakuwa wao ndo waasisi wa Taifa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI