Na Mbaruku Yusuph,Matukio Daima APP Handeni
JAMII za kifugaji toka Ngorongoro zilizohamia Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni zimetakiwa kupuuza uzushi unaonezwa na vyama vya upinzani juu ya uminywaji wa uhuru wa kufanya matamasha ya kuenzi mila na desturi zao
Kauli hiyo imetolewa Sept 23 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman kwenye Tamasha la kuenzi mila, tamaduni na desturi ya jamii ya Kimasai na kusema kuwa Serikali inatakeleza ilani ya Chama hicho kwa wananchi wote.
Alisema Chama hicho kiliielekeza Serikali kuzingatia utu wa kila Mtanzania bila ya kuangalia itikadi za vyama,dini na makabila na ni tofauti na uzushi unaonezwa na vyama hivyo vya upinzani ya kuwa Serikali inaminya uhuru wa jamii hiyo kufanya matamasha yao ya kimila.
Rajabu ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa alisema awali Serikali ilipowahamishia Msomera wafugaji hao yapo madai yalizushwa ya kutokuwepo kwa huduma za kijamii jambo ambalo lilitekelezwa na Serikali kwa kiwango bora ambacho hakikutarajiwa.
"Walisema hakuna huduma za kijamii lakini sasa kila kitu kipo shule,minara ya simu,maji,barabara,umeme,ofisi ya posta na hata kituo cha Polisi sasa wameanza kuzungumzia matamasha ya kimila pia yanafanyika na leo kila mtu atakuwa shahidi hapa "Alisema Rajabu.
Rajabu ambae amepewa jina la OLORETISHO na jamii hiyo ya Kimasai jina lililokuwa na maana ya "mtu ambae anasaidia jamii kutatua matatizo"alisema anatambua wapinzani hao wa Chama ndio wapinzani wa Serikali na kama wamekosa hoja milango ipo wazi wajiunge na ccm kwa maslahi ya kuwasaidia na kuwatumikia wananchi.
Hata hivyo alitoa angalizo kwa Viongozi wa Serikali toka Wilaya zote za Kilindi na Handeni waache kuwa chanzo cha kuanzisha mgogoro wa kukigombania Kijiji hicho cha Msomera na hatua kali zitachuliwa dhidi yao bila ya kuangalia nafasi zao.
Kwa upande wake Mkuu Wilaya Handeni Wakili Msomi Albert Msando alisema katika awamu ya kwanza Serikali imejenga nyumba 500 kwa ajili ya wafugaji hao wanaohama kwa hiari toka katika hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia Kijijini hapo.
Wakili Msando alisema kutokana na jamii hiyo kuonyesha nia nzuri ya kupisha uhufadhi na kutaka kuondoka Ngorongoro ili wahamie Kijijini hapo Serikali imedhamiria kujenga nyumba 5,000 ambazo zitajengwa katika Wilaya tatu Handeni, kilindi na kiteto kwa ajili ya jamii hizo za kifugaji.
Aidha alisema matarajio ya ujenzi wa nyumba hizo kwa ajili ya jamii hizo za kifugaji utachukua miezi sita ambapo matarajio kumalizika mwezi Machi 2024 na nyumba hizo zitagharimu Bil 260 na kuongeza kuwa Watanzania wanajitambua kwa Utanzania wao na sio ukabil,dini wala mila zao.
Ruth John mwanachi wa jamii hiyo ya kimasai muhamiaji toka Ngorongoro alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwapa makazi ya kudumu sambamba na umiliki halali wa ardhi kwa ajili ya makazi,kilimo na ufugaji tofauti na walupokuwa wakiishi huko Ngorongoro.
Ruth alisema baada ya kutambua umuhimu wa uhifadhi wa mbuga ya Ngorongoro na wanyama waliopo ambayo inafaida kwa Watanzania wote kwa hiari yao wameona njia pekee ya kuihifadhi ni jambo jema wahamie katika Kijiji hicho cha Msomera ili kuepusha uharibu unaofanywa na wafugaji wanaoishi katika mbuga hiyo.
0 Comments