UN WOMEN yahamasisha Wanawake wa Wilaya tatu za mkoa wa Pwani kushiriki uchaguzi iliwapate uongozi kwaajili ya chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji mwakani na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo Mratibu wa Mafunzo Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Kibaha Mji Maria Nkangali amezitaja Wilaya zitakazonufaika na Mafunzo hayo kuwa ni Kisarawe, Chalinze na Kibaha Mji ambapo Mafunzo hayo pia yamehusisha makundi mbalimbali wakiwemo Watu wenye ulemavu, wazee wa Mila na Walimu.
Amesema sababu za kutoa Mafunzo hayo ni kutokana na Mwitikio Mdogo wa Wanawake kushiriki Katika Chaguzi za Uongozi mbalimbali.
Amesema Mafunzo hayo yatawaibua Wanawake Wengi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji wa mwakani ikiwa ni pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Kata za Halmashauri ya mji wa Kibaha kwa ushiriano wa uongozi wa Halmashauri hiyo ambapo UN WOMEN hupata nafasi ya kuzungumza na Wananchi katika Kata za Pangani, Mkuza na Visiga.
Wakiwa katika Kata ya Visiga wamehamasisha Wanawake hao kwa kuzungumza na Wananchi wote bila kujali jinsia zao wakiwapatiwa Mafunzo ya namna ya Ushiriki wa Wanawake na Wasichana Katika Uongozi na Haki za kiuchumi kwa Wanawake.
Aidha Kwa upande wake Mratibu Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkaminoela Hangaya amesema Katika majukwaa hayo Wanawake Wengi hawana Elimu ya Biashara hivyo majukwaa hayo yatasaidia kuwakwamua kiuchumi.
0 Comments