Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROF PATRICK NDAKIDEMI ASHIRIKISHI KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA OLDMOSHI MAGHARIBI

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameshiriki katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Oldmoshi Magharibi katika vitongoji vya Osungura na Kirembeni. 


Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, uchaguzi huo utafanyika Septemba 19 mwaka huu.



Kampeni hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Makao Makuu Dodoma, Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Moshi Vijijini. Pia walikuwepo wawakilishi wa  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania.



Uchaguzi huo utafanyika ili kukamilisha safu ya uongozi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Menyasumba Macha.



Akiongea kwa nyakati tofauti, Ndakidemi alimuombea kura Peter Massawe na kuwaomba  wananchi  waliohudhuria katika mikutano hiyo kwamba, kwa unyenyekevu mkubwa anawaomba wamchague mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili akaungane naye kwenye kuitekeleza ilani ya CCM.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI