Header Ads Widget

SEKTA YA BIMA YAZIDI KUKUA TANZANIA

 

Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 

Sekta ya Bima nchini Tanzania imezidi kukua na kuongeza patoa la Taifa kwa kipindi cha miaka mitano ambapo mauzo ghafi ya bima yameongezeka kutoka shill bill 691.9 kwa mwaka 2018 hadi kufikia takriban shill trill 1.2 mwaka 2022.


Kauli hiyo, imetolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari ambapo amesema sekta ya bima imekua kutoka asilimia 0.56 kwa mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 1.68 kwa mwaka 2021 ambapo Mamlaka ya Bima (TIRA) imeongeza  gawio Serikalini kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 kwa shilingi bilioni 2.9.


Aidha, amesema malipo ya madai na mafao ya bima za maisha yameongezeka kwa asilimia 29.3 kutoka Sh bilioni 95.7 mwaka 2021 hadi bilioni 123.71 mwaka 2022,jumla ya kiasi cha madai kilicholipwa mwaka 2022 ni Sh bilioni 455.80 hivyo, kupunguza umaskini kwa wanufaika na kufanya biashara.


Hata hivyo, amesema katika eneo la kulinda haki ya mteja wa bima, Mamlaka hiyo imeendelea kuzisimamia kampuni za bima kuhakikisha zinalipa madai na fidia stahiki kwa wakati na kwa haki.


"ulipaji wa madai na fidia stahiki kwa wateja wa bima umefikia asilimia 95 hivyo kupungua kwa malalamiko toka kwa wananchi ambapo asilimia tano ya madai na fidia yana changamoto ambazo TIRA inafuatilia na kutoa suluhisho, mfano, ulipaji wa madai ya bima za kawaida umeongezeka kwa asilimia 10.1 kutoka Sh bilioni 301.9 mwaka 2021 hadi Sh bilioni 332.09 mwaka 2022"amesema Dkt.Saqware.


Sambamba na hayo amesema kuhusu mafanikio ya TIRA, katika kipindi cha mwaka wa Fedha wa 2022/2023 Mamlaka imeanzisha Konsotia (Umoja) ya Bima ya Kilimo ili kutekeleza skimu ya bima ya Kilimo Tanzania kwa ufanisi.


Ameongeza kuwa TIRA pia imeanzisha Konsotia ya Bima ya Mafuta na Gesi ili kuhakikisha miradi yote ya gesi na mafuta inabakiza sio chini ya asilimia 45 ya ada zitokanazo na gesi na mafuta.


"Kufuatia kutokuwa na uwezo wa soko la ndani, vihatarishi vya nishati, vilielekezwa nje ya Nchi kwa asilimia 100. Jambo ambalo sio na lisilo na tija kwenye uchumi wa nchi" ameongeza Dkt. Saqware.


Hata hivyo, amesema kuanzishwa kwa miradi mikubwa ya nishati kama vile bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ni fursa kwenye sekta ya bima kujipanga kwa ajili ya kuongeza tija, uchumi na ajira nchini na kutoa fursa kwa kampuni za bima za ndani kushiriki na kuandika vihatarishi vya nishati ya Gesi na Mafuta ndani ya nchi.


Amesema mpaka sasa kampuni 22 za Bima zimesaini Mkataba wa Muungano huo wa Bima ya Nishati ya Mafuta na Gesi Tanzania zenye jumla ya laini (hisa) 238 ambapo kila laini (hisa) ina thamani ya Dola za Kimarekani (USD) 25,000 ambayo ni jumla ya uwezo wa muungano wa kiasi cha mtaji cha dola za Marekani milioni sita.


Ameongeza kuwa, katika mwaka wa fedha 2023/24 TIRA imeanzisha mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi ili kuifanyia marekebisho sheria ya Bima na Kanuni zake kufuatia maboresho ya mifumo ya usimamizi wa Bima na maendeleo ya soko la bima nchini ambapo wamelenga kukusanya maoni angalau ya wadau 500.


Dkt. Saqware amesema mamlaka hiyo imepanga kuanzisha na kutekeleza Mpango wa kitaifa wa Bima ya Kilimo na kuanzisha bodi ya wataalamu wa Bima, Hifadhi ya Jamii na Takwimu Bima pamoja na kuunganisha mifumo ya kidigitali na Taasisi za umma ikiwemo Jeshi la Polisi, LATRA, NIDA, TASAC, TRA, PTA, ZRA lengo likiwa ni kuongeza usimamizi na maendeleo ya soko la Bima.


TIRA pia itaendelea na utoaji wa elimu ya bima kwa umma na wadau mbalimbali. “Kwa mfano Mamlaka imeandaa Semina ya Pili ya Makatibu Wakuu wote Nchini kwa lengo la kutoa elimu ya umuhimu wa ukataji bima. Semina imepangwa kufanyika Oktoba 27, 2023,”


Pamoja na hayo, amesema mamlaka hiyo itafungua ofisi za Bima Mtawanyo za Kikanda ambazo Serikali ya Tanzania inamiliki hisa za moja kwa moja au kupitia Taasisi zake ili kampuni hizo ziweze kufungua ofisi nchini kwa utaratibu wa Mikataba ya Uenyeji ili kuwa na soko la Bima lisilokuwa na udanganyifu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI