Header Ads Widget

MWANADIPLOMASIA MKUU WA CHINA KUITEMBELEA URUSI.

Na Simon Joshua - Matukio Daima App, China.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China Wang Yi anakwenda Urusi leo kwa ziara ya siku nne ambayo ajenda kuu itakuwa mazungumzo kuhusu usalama, ikiwa ni mwendelezo wa mashauriano ya ngazi ya juu baina ya pande hizo mbili.


Beijing imesema mwanadiplomasia huyo mkuu ataitambelea Moscow kushiriki duru ya 18 ya mashauriano ya kimkakati kuhusu ulinzi kati ya Urusi na China kwa mwaliko wa Katibu Mkuu wa Baraza la Ulinzi wa Taifa nchini Urusi, Nikolai Patrushev.


Mwezi uliopita Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu alizitembelea Urusi na Belarus na kutoa mwito wa ushirikiano zaidi wa kijeshi.


Katika miezi ya karibu China na Urusi ambazo ni washirika wa kimkakati zimefanya luteka za pamoja za anga na baharini .


Mahusiano yao yameimarika zaidi tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari mwaka jana, kitendo ambacho hadi sasa China haijakilaani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS