MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud ameagiza kufungiwa kwa Baa ya Nice Beach Resort kufuatia Malalamiko yaliyotolewa na Wananchi juu ya ukiukwaji wa Sheria na maadili.
Ayoub ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano maalumu wa kusikiliza Kero mbalimbali kwa shehia Tatu ikiwemo Shehia ya Mangapwani, Misufini pamoja na Kidanzini katika Uwanja wa Vidimni.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua hiyo ameichukua kufuatia kero zilizotolewa na Wananchi na kujiridhisha juu ya ukiukwaji wa Sheria, taratibu na maadili.
"Kupitia kikao hichi ndugu zangu Wananchi nataka kuwaambia kuwa baa imekiuka taratibu, Sheria na maadili yetu hivyo namwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa kuifungia baa haraka iwezekanavyo," Ameeleza.
Kupitia Kikao hicho Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza Wamiliki wa Baa na kumbi za Starehe kufuata kanuni na Sheria za Nchi.
0 Comments