Header Ads Widget

KUWASA KUENDESHA OPERESHENI KAMATA WEZI WA MAJI

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 


MAMLAKA ya maji safi na maji taka Kigoma Ujiji imetangaza kuendesha operesheni maalum ya kukamata watu wanaojiunganishia maji bila kufuata taratibu jambo linaloitia hasara mamlaka hiyo.

 


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Poas Kilangi akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma alisema kuwa mpango huo unakuja kufuatia ziara aliyofanya ambayo amegundua kuwepo kwa wizi na uchepushaji maji unaofanywa katika maeneo mbalimbali mtaani kwenye manispaa ya Kigoma Ujiji.



Kutokana na hali hiyo Mkurugenzi huyo ametoa wiki mbili kwa watu wote wanaotumia maji bila kufuata taratibu (wezi)  kujisalimisha kwa uongozi wa mamlaka hiyo kwani  baada ya muda huo mamlaka itachukua hatua za kisheria  kwa watu wote watakaobainika kufanya kosa hilo.

 



Katika hatua nyingine Kilangi amewataka wateja wanaotumia maji yanayozalishwa na malaka hiyo hasa nyumba za ibada, masoko na mitaani kutumia maji hayo vizuri kuepuka matumizi makubwa yasiyo na tija ambayo yanawafanya kulipa bili kubwa.


Akizungumzia operesheni hiyo ya KUWASA Mratibu wa Shirika la Nyakitonto Youth Development, Ramadhani Joel alisema kuwa shirika lake kwa kushirikiana na KUWASA liliendesha mradi wa uwajibikaji kwa watendaji wa mamlaka hiyo kusikiliza kero za wananchi na upande wao wananchi kushirikiana na mamlaka kusaidia mivujo na  wizi wa maji.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI