Header Ads Widget

AKINA MAMA NJOMBE WAELIMISHWE JUU YA UDUMAVU KWA WATOTO.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka
Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Mhe.Deo Mwanyika
Mnenaji mkuu wa Wasabato Mchungaji Richard Mashauri

xxxxxxxxx

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati elimu mbalimbali zikiwemo za afya na lishe zikitolewa kwa waamini wa dhehebu la waadvetista wasabato kupitia sherehe za makambi mjini Njombe,akina mama wametakiwa kutumia muda wao kuwalea vyema watoto badala ya kuwasahau na kujikuta wanakumbwa na changamoto ya lishe ukiwemo udumavu na utapiamlo.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka wakati wa kufunga makambi hayo amewataka akina mama kutenga muda kwa ajili ya kuwalea watoto ambao wamekuwa na utapiamlo na ukondefu unaosababisha mkoa  kuingia kwenye rekodi mbaya ya udumavu.


Nao wachungaji wa dhehebu hilo akiwemo Mnenaji mkuu Mchungaji Richard Mashauri wamesema kwa wiki nzima mwamko umekuwa ni mkubwa katika kueneza neno la mungu pamoja na kuwaasa wananchi kuepukana na matukio ya kihalifu na mauaji.


Deo Mwanyika ni mbunge wa jimbo la Njombe mjini ambaye naye amewataka wazazi kushirikiana katika malezi ya watoto ili waje kulisaidia taifa.


Kwa upande wao wazazi akiwemo Faines Mkarabi wamekiri kwenda kufanyia kazi changamoto ya malezi ya watoto ili waje kuwa na akili katika maisha yao.


Kwa mujibu wa waziri wa afya nchini Tanzania Ummy Mwalimu kupitia taarifa aliyoitoa februari 7 mwaka huu alisema mkoa wa Iringa unaongoza kwa udumavu kwa asilimia 59.9,Njombe asilimia 50.4 na Rukwa kwa asilimia 49.8.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI