Na Mwandishi wetu Lindi
Watanzania wahamasishwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo ili kuboresha kilimo nchini.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Grace Lemunge alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa kwa lengo la kuhamasiha uwekezaji nchini hivyo watanzania wanahamasisha kuona fursa hiyo muhimu.
Alisema kuwa mpaka sasa kituo hicho kina taasisi 12 ambazo husaidiana nazo ili kuhakikisha kuwa mwekezaji hapati changamoto wakati anapohitaji kuwekeza katika sekta yoyote.
“Unajua hiki kituo kilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji hapa nchini sisi kama kituo tunazo taasisi 12 ambazo zinasaidia uwekezaji kufanyika hapa nchini ikiwa ni pamoja na Brella kwenye usajili wa kampuni, kupata vibali vya mazingira NEMC, timu ya TANESCO kwaajili ya umeme tuna TRA TIN na malekezo mbalimbali ya tunao TMDA na TBS vyote ni kusaida watanzania huduma zote zinapatikana katika dirisha moja” alisema Lemunge
"Alisema kuwa zipo sekta nyingi lakini tunayo sekta kipaumebele ambayo ni kilimo mazao mbalimbali tunahamasisha uchakataji wa mazao ili mradi kuanzisha kiwanda.
“Tumekuja kuahamasisha watanzania takwa la usajili limeshuka kutoka dola laki 1 hadi 50 ambapo mtanzania akiwa na dola milioni 100 anaweza kusajiliwa na kituo chetu ni vema watanzania tumieni fursa ya uwekezaji nchini”
“Ili wawekezaji wasihangaike kwenda kutafuta vibali katika maeneo ya mbali tumerahisisha vibali vyote vinapatikana hapa pia tunahamasishsa uwekezaji wa viwanda hususani vya kilimo tumeweza kusajili miradi mbalimbali” alisema Lemunge








0 Comments