Wakulima wa zao la mbaazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwakutumia mbegu bora za muda mfupi zilizofanywiwa utafiti na TARI ili kuondoka a na mbegu za muda mrefu zisizo na tija.
Akizungumza na wakulima Mtafiti wa mazao jamii ya mikunde Dr John Tenga alisema kuwa kitendo cha Mfumo wa stakabadhi ghalani kuaanza kufanyakazi kitasiaidi wakulima kupata bei nzuri na pia itasaidia watafiti kupata takwimu halisi za uzalishaji wa zao hilo.
"Unajua hata udongo wetu kusini unauwezo wa kulima mbaazi tumejaribu kuhamasisha kulima kwakutumia mbegu bora zinazozaa kwa muda mfupi zikiwa na mazao mengi"
"Zamani wakulima walitumia mbegu za asili ambazo zilikuwa zinachukua miezi nane lakini baada ya utafti mbegu zimekuwa za muda mfupi zina zaa sana katika kipindi cha miezi 5-6.
“Tunazo aina nne za mbaazi Ilonga1&2, Tumia na Komboa ambazo zinazaa kwa muda mfupi ili kumuhamasiha mkulima kulima zao hilo ingawa wapo wakulima ambao zamani walikaa na kusubiri katika kipindi cha miezi 8 ili zikomae”
"Wakulima wengi wanalima unajua kilimo cha kusubiri mizie nane na ukasikia miezi 5 wengi wamechukua na wanalima kwa wingi zaidi"alisema Dr Tenga






0 Comments