Header Ads Widget

MEJITII AFURAHISHWA NA UTAYARI WA WAKULIMA KUWA WABUNIFU

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na Mjumbe wa Halmashauri kuu  Taifa CCM mkoa wa Dodoma Donald Mejitii amekiri kufurahishwa na utayari wa wananchi ambao ni Wakulima kwa kuwa wabunifu kupitia mazao ya ndani kwa kuongeza mazao mnyororo wa thamani.


Amesema hayo jijini Dodoma Wakati alipokuwa akitembelea mabanda katika sherehe zinazoendelea za maonesho ya Wakulima na wafugaji Nzuguni  Dodoma.


"Nimefurahishwa kuona mazao yameongezewa thamani kwani huko nyuma tulikuwa tukivuna mavuno kutoka shambani na kupeleka sokoni lakini Sasa mambo yamebadikika ambapo tunaona Alizeti mchakato wake unaleta sabuni ,mkaa mafuta ya kupaka ni mambo makubwa huku nyuma hayakuwepo,"Amesema Mejitii


Amesema Kupitia awamu ya mikopo ya Halmashauri vikundi vingi vimepata mikopo ya asilimia 4 vijana na akina mama wamewezeshwa ambapo mafanikio kwa vijana na Wanawake ni makubwa.


"Hivyo jamii kuanza kutumia bidhaa zinatengenezwa na wajasiriamali Kupitia mazao wanayoongezea mnyororo wa thamani," Amesema Mejitii


Aidha amesema zipo bidhaa nyingi zinazotokana na kilimo hivyo ni wakati sasa kwa tanzania kutumia bidhaa hizo kutoka kwa wajasilimali wetu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI