Header Ads Widget

WAKULIMA WAHAMASISHWA KULIMA MBEGU BORA ZA UFUTA

 



 Na Mwandishi wetu, Lindi


Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele Mtwara wamewahamasisha wakulima kupanda mbegu Bora zinazofanya vizuri sokoni ili kuondokana na tatizo la bei sokoni huku akishauri Kutoa oda ya mbegu mapema. 

Kauli hiyo ameitoa katika banda la maonyesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi Mtafiti wa Zao la Ufuta kutoka TARI Naliendele Zabron Ngamba alisema kuwa wakulima wa ufuta nchini wanalima kwa wingi lakini wanaotakiwa kulima zao hilo kwa tija ni vena vyama vya Ushirika vikawekeza kwenye hili. 


“Tunapawa kupeleka sokoni kilicho bora ili kupata mazao yenye tija yatakayouzika sokoni bila changamoto yoyote hiyo ndio itaboresha wakulima wetu kuanzia kwenye kipato na kuwajengea uwezo wa kujiamini pia kwakuwa watakuwa wampanda mbegu Bora wanasubiria mavuno Bora kuelekea kwenye mbegu bei bora"



“Ili kupata Bora vyama vya Ushirika vinamchango mkubwa kuwajenga wakulima na kuwapatia mbegu sahihi kwa wakati sahihi ili kupata mavuno kwa wakati sahihi"


Mussa Jabir mkulima wa ufuta Lindi  wapo wakulima wengi wanahitaji elimu hii ili kuboresha Kilimo hiki pamoja na kuongeza hamasa ya kulima ufuta Bora wenye soko kubwa duniani.


“Nimejifunza mengi kuanzia kujua mbegu Bora upandaji namna bora ya upogoleaji nimevutiwa na Somo hili naamini nikiweza kulima na kupata ufuta mwingi Sina haja ya kuuza na weza kamua mafuta na kuyauza yaani kuongeza thamani"



Mratibu wa Uhaurishaji wa Teknolojia na Mahusiano wa kituo cha Tari Naliendele Rashid Kidunda Alisema kuwa wamekuwa wakifanya tafiti za mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wakulima wa mazao ya Korosho, karanga na ufuta wanapata mbegu Bora zenye matokeo sahihi shambani.


“Tunafanya tafiti za mazao mengi ili kuweza kuwasogezea huduma wakulima ambao tuko nao kwenye kanda hii ya Kusini kwakushirikiana na vituo vingine vya TARI” alisema Kidunda


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI