Header Ads Widget

RC LINDI AHAMASISHA ULAJI NA UBANGUAJI WA KOROSHO





Na Mwandishi wetu, Lindi.


Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack  amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kula bidhaa zitokanazo na korosho ili kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini vya ubanguaji wa korosho ambapo utaongeza ajira nchini.


Akizungumza wakati wa KOROSHO DAY iliyoandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania CBT kwakushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele  alisema kuwa siku hiyo ni maalum kwaajili ya kuhamasisha ulaji wa ambazo zinazlishwa nchini ulaji wa korosho na mabibo pamoja na bidhaa zitokanazo na korosho zinafaida kubwa kwa afya ya miili yetu.


"Kuna maziwa ya korosho na siagi hutupatia ambayo virutubisho vya protin wanga  na mafuta kwa wingi pia madini joto ya chuma, maginiziam, copper ambayo huimarisha mifupa na seli kwa wingi wakati mabibo ya korosho na bidhaa zake hutupatia vitamin C  kwa wingi mara tano ya inayopatikana kwenye machungwa na mbogamboga ambayo inasaidia kulinda mwili” 


“Ni vema tukahamasisha watananzia kula korosho kwaajili ya afya zetu ndio maana tunaitangazia dunia kuwa kusini tunalima korosho na tunatamani tusiwapelekee wenzetu kula tuanze kula sisi alafu zinazobakii ndio tupelekee wenzetu” 



“Wenzetu wananunua tani kwa tani za korosho wanapeleka kwao kwanini tusijiulize kwanini wananunua na wanapata nini hicho wanachpata kwanini sisi tusipate kupitia korosho nasisi tujikite kwenye kubangua na kula ili nasi tunufaike na faida hizo”


 “Pia inasaidia kuongeza na kuimarisha soko la ndani kupitia ongezeko la ulaji wa korosho kutawezesha wajasiliamali na wawezekezaji  kujikita katika kuongeza mnyororo wa thamani ambapo kwenye ubanguaji bado tuko chini tunabangua chini ya asilimia 10 tu”


kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Bri.Gen. Mstaafu Aloyce  Mwanjile amesema kuwa  leo ni siku muhimu ya ulaji wa korosho ambayo ni mahususi kwaajili ya kuhamamsisha watu kula korosho ili kuondoa dhana ya kuwa  kuwa tunalima ili tuuuze nje ya nchi.



Alisema kuwa mawazo hayo utusahaurisha  kuwa kuna mazao mengi yatokanayo na korosho ambayo tukiyatumia yataleta virutubisho katika miiili yetu. 


Mratibu wa Uhaurishaji wa Teknolojia na Mahusiano kituo cha Tari Naliendele Rashid Kidunda  alisema kuwa tunalo jukumu la kuzalisha mbegu bora za korosho  na kubaini magonjwa na wadudu wa haribifu na mbinu za kudhibiti.


“TARI kwakushirikiana na CBT katika maonyesho ya nanenane tumekuwa tukiratibu ya  siku ya korosho ambapo wadau mbalimbali na wananchi hupata fursa ya kula na kunywa korosho bila gharama yoyote lengo ni kuhamasisha uwekezaji katika uongezaji thamani wa korosho  pamoja na mabibo” 





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI