NA THABIT MADAI, ZANZIBAR - MATUKIO DAIMA APP
WADAU wa Michezo Visiwani Zanzibar wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Ussi Salum Pondeza kwa jitihada anazozifanya za kuibua na kukuza Vipaji vya Vijana katika Michezo mbalimbali kwa kuandaa mashindano ya Jimbo pamoja na Msaada wa fedha na Vifaa vya Michezo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mara baada ya Mchezo wa Nusu Fainal ya kwanza katika Tamasha la Michezo la Jimbo la Chumbuni, Kiongozi na Mchezaji wa Timu ya Karakana FC Haji Abdarham Hilma amesema kuwa Mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya Timu mbalimbali ndani ya Jimbo hilo.
"Nimshukuru sana Mbunge wetu, Mhe Pondeza kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza vipaji vya michezo ambapo kwa Timu yetu amekuwa akitoa msaada mbalimbali," amesema.
Ameongeza kuwepo kwa Mashindano mbalimbali katika Jimbo la Chumbuni kunapelekea kuibua Vipaji vingi vya Vijana katika maeneo yao.
Nae Nahonda wa Timu ya Chumbuni Abdallah Haji amesema kuwa, anamshukuru Mbunge wa Jimbo la Chumbuni kwa kuanzisha matamasha mbalimbali ya Mchezo ambayo yana lengo la kuibua Vipaji vya Vijana na kuwaendeleza.
"Mimi Binafsi nmshukuru Mbunge kwa Tamasha hili limetuonesha Vipaji vingi tulivyojaaliwa katika Jimbo letu, sasa niwaombe Wananchi kuweza kujitokeza kushirikia maana vipaji vinaovyonekana vinaendelezwa," amesema.
Hata hivyo Nahondha huyo ameelezea furaha yao mara baada ya kushinda kwa mikwaju ya Penati na kufanikiwa kuingia fanaili katika Tamasha hilo la Michezo.
Ameeleza kuwa Wamejipanga kuweza kuchukua Ubingwa na Pondeza Chumbuni Festival kwa mwaka 2023.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Ussi Salum Pondeza amesema kuwa, dhamira kubwa ya kuanzisha Matamasha katika Jimbo hapo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya kufanya Michezo kuwa Ajira kwa vijana.
"Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM inasema Michezo ni Ajira hivyo kwa kuliona hilo tumeamua kuanzisha Tamasha ili kuwafanya Vijana wanufaike na Vipaji walivyo nvyo katika michezo mbalimbali," amesema.
Aidha amesema kuwa ataendelea kusaidia Timu mbalimbali kwa kuwapatia Vifaa vya Michezo pamoja na Fedha Taslimu ili kuziimarisha Timu za Michezo zilizopo katika Jimbo la Chumbuni.
Nusu fainali ya Pili inatarajiwa kuchezwa siku ya Kesho katika Uwanja wa Saateni ambao utawakutanisha Mwembe Makumbi juu na Mwembe Makumbi chini ambapo Michezo Mingine itachezwa katika Kilele cha Pondeza Chumbuni Festival.
0 Comments