Na Eliza Ntambala,Matukio Daima App,
Nsimbo
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe ambapo alitoa wito kwa wauguzi kuacha tabia ya kuwapa majukumu wanawake ya kuchota maji pindi wanapokwenda katika vituo afya na zahanati za serikali kujifungua.
Ukosefu wa maji safi salama kwa baadhi ya vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi ni chanzo cha wanawake wajawazito wanaokwenda kujifungua kupewa jukuma la kuchota maji.
Baadhi ya wanawake wakitoa kero zao hivi karibuni kwa mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe wameeleza kuwa wanapopata uchungu na kwenda katika zahanati za serikali baada ya kujifungua na kabla hawajaruhusiwa kurudi nyumbani wanatakiwa kuchota ndoo tano za maji ikiwa kwa wakati huo hawajapata nguvu.
0 Comments