NA THABIT MADAI,ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema kwamba, itahakikisha inasimaia ipasavyo Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa katika Mchezo wa Ngumu kwa lengo la kulinda haki na Maslahi ya Mabondia.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla fupi ya upimaji wa Afya kwa Mabondia zaidi ya 14 kutoka Zanzibar na Bara kuelekea katika Usiku wa Masumbwi Agost 27 mwaka huu.
Amesema kuwa Serikali imejipanga vyema katika kusimamia Sheria, kanuni na taratibu ili kulinda Haki na Maslah ya Wapigani pamoja na kuhakikisha mchezo wa ngumi haupiganwi kiholela.
"kwaiyo Serikali ipo karibu na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Zanzibar ambapo tutasisimimia ipasavyo Sheria, Kaununi na Taratibu zote ili Mchezo huu uchezwe kwa utaratibu maalum kama sehemu nyngine zinzvyocheza mchezo huu," amesema.
Mapema Afisa Uhusino wa Tosh Sport Matlida Peter amesema kuwa maandalizi kuelekea Usiku wa Masumbwi Zanzibar Agost 27 yamekamilika ambapo Mabondia Tayari wameshapimwa Afya na vituo vya Uuzwaji wa Tiketi tayari vimeshatangazwa.
Kwa upande wao Mabondia akiwemo Dulla Mbabe na Said Hamadi wameeleza kuwa, Zoezi la upimaji wa Afya limekwenda vizuri kinachosubiriwa ni siku ya Mapambano ambapo wameahidi kutoa Burudani.
0 Comments