Header Ads Widget

PONDEZA CHUMBUNI FESTIVAL KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA

 


NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP

MBUNGE wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza amepongeza Muitikio wa Wananchi katika Tamasha la Michezo la Jimbo hilo ambalo lina lengo la kuwaunganisha pamoja Wananchi pamoja na kuibua fursa na Vipaji vya Vijana.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza amesema lengo la Tamasha hilo la Mchezo ni kuwaunganisha Wananchi katika jimbo hilo huku likibeba ujumbe mbalimbali wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Amesema, Katika Tamasha hilo ambalo limebeba jina la Pondeza Chumbuni Ferstival litakuwa muendelezo kwa michezo mbalimbali ambapo washindi watakabidhiwa Fedha Taslim.


"Tamasha hili limelenga kuibua, kukuza vipaji vya Vijana wenu hapa jimboni lakini pia kuwapatia fursa mbalimbali za Ajira," amesema.


Mapema, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Pondeza Chumbuni Festival Makame Sufiani amesema kuwa Mashindano hayo yanajumuisha Timu kutoka Jimboni hapo ambapo michezo inacgezwa kwa njia ya mtoano.


Pondeza Festival imeandaliwa na Taasisi ya Pondeza Foundation ikiwa na lengo la kuwaunganisha Wananchi katika Jimbo la Chumbuni

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI