Header Ads Widget

TUSIWATENGE WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU-KATIMBA

 



Na Editha Karlo,Kasulu

MBUNGE  wa viti maalumu kundi la wanawake mkoa wa Kigoma Zainab Katimba ameitaka jamii kujali na kuthamini watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwagusa kwa namna mbalimbali.


Katimba ametoa wito huo wilayani Kasulu mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea na kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Kabanga Mazoezi na kusisitiza kuwa kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kuguswa na mahitaji ya kundi hilo.


" Tunapaswa kuelewa kwamba hakuna binadamu ambaye ni muhimu zaidi ya mwingine wote tupendane na nimefurai kukuta watoto wenye mahitaji maalumu wanasoma pamoja na wototo wengine hii inasaidia sana kujenga kizazi chenye kujali na upendo.,,



Aidha mbunge huyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuanzisha kituo hicho ambacho mpaka sasa kina watoto wenye mahitaji maalumu miamoja hamsini na moja (151 ) na kusisitiza kuwa uwepo wa huduma hiyo utalowezesha kundi hilo kutimiza ndoto zake kupitia fursa ya elimu.


"Na niwambie wadogo zangu nyie nu watu muhimu sana someni kwa bidii ili baadaye mtimize ndoto zenu ,ninvyowatazama hapa wanaona mawaziri ,wabunge madaktari walimu na kada nyingine,, amesema Mh,Katimba.

 

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Happiness Boy amemueleza mbunge huyo kuwa pamoja na kuendelea kufanya vizuri kituo hicho kinakabiliwa na changamoto kadha zikiwemo ufinyu wa bajeti ya chakula kwa wanafunzi wa bweni na upungufu wa wa walimu wa elimu maalumu.



Mbunge huyo ambaye yupo katika ziara inayolenga kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii pia ametembelea hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu na kutoa zawadi mbalimbali kwa wanawake waliojifungua .


Akiwa hospitalini hapo Katimba pia ametembeleo jengo la wagonjwa mahututi ambalo limegharimu zaidi ya milioni miambili hamsini na kumshukuru rais Dkt ,Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuimarisha sekta ya afya nchini


" Hakika mheshimiwa rais anafanya kazi kubwa sana na matunda yanaonekana si kwenye afya tu mfano tumeona kwenye elimu maji na hata miundombinu .alisema Mh,Katimba.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI