Na,Jusline Marco;Arusha.
Spika wa bunge la Baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulidi amesema kwa kipindi chwa 2022/23 serikali ya Tanzania iliweka nguvu kubwa kwenye katika kuboresha kilimo na mifugo ambapo mikoa ya kanda ya kaskazini imenufaika na mamno mbalkmbali ikiwemo utolewaji wa mnolea za ruzuku kwa ajili ya kuongeza tija kwenye kilimo.
Mhe.Maulidi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua maonyesho ya wakulima nanenene yanayofanyika Katika viwanja vya themi jijini Arusha ambapo amesemankwa mwaka wa fedha 2022/23 jumla ya Tani 17288 zimetolewa kwa mkoa wa Arusha na kuwanufaisha wakulima 19663 na Tani 18557 zimetolewa kwa mkoa wa Kilimanjaro na kuwanufaisha wakulima 62829 huku Mkoa wa Manyara ukipata Tani 4840 na kinufaisha wakilima 6829.
Ameongeza kuwa uanzishwaji wa mashamba darasa ya malisho katika Mikoa mitatu ya Kanda ya Kaskazini kwa lengo la kuhakikisha usalama wa malisho kwa mifugo kwa Mkoa wa Arusha wamepata jumla ya mashamba darasa 3 ,Kilomanjaro mashamba darasa 3 na Manyara wamepata mashamba darasa 3,huku ujenzi wa majosho ya mifugo na kutoa dawa za kuogesha kwa lengo la kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe ambapo jumla ya majosho 5 yamejengwa kwa Mkoa aa Kilimanjaro,majosho 4 kwa Mkoa wa Manyara na majosho 4 kwa Mkoa wa Arusha.
Aidha ameeleza kuwa jumla ya pikipiki 245 zimetolewa kwa mkoa wa Kilimanjaro,pikipiki 191 kwa mkoa wa Manyara na pikipiki 210 kwa mkoa wa Arusha ili kuwawezesha maafisa ugani kufanya shughuli za ugani kwa urahisi na kuwafikia wakulima wengi zaidi huku uanzishwaji wa viwanda vya mazao ya mifugo vikianzishwa na uboreshwaji wa miundombinu ya umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa mvua katika kukuza mazao ukifanyika.
Vilevile amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiako kwa serikali ili iweze kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapk amesema maonesho hayo yana lenho la kuonyesha fursa zilizopo katika sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kutoa elimu kwa wakulima,wafugaji na wavuvi ili uzalishaji wa mazao na bidhaa zinazotokana na sekta hizo uwe na tija na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ameongeza kuwa kauli ya mwaka huu ya "Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula "pamoja na mambo mengine inalenga kuwaonesha watanzania kwamba vijana na wanawake ni kundi kubwa la watu wenye ushiriki na mchango mkuwa kwenye kilimo,mifugo na uvuvi na katika kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda na kuongeza thamani ya mazao na upatikanaji wa masoko ndani na nje ya nchi yenye maslahi kwa wakulima,wafugaji pamoja na wavuvi.
Kwa upande wake Afisa uwekezaji Kanda ya Kaskazini Bwn.Valentine Vedasto Kagombora kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania katika Maonesho hayo amesema kuwa pamoja na jukjmu la usajili wa miradi kutoka kwa wawekezaji pia wanatoa vyeti kwa wawekezaji lengo likiwa ni kupunguza gharama za uwekezaji nchini.
Bwn.Gahombora amesema pia TIC wanazo program za kuwainua wakulkma wadogo na kuwaunganisha na wafanyabiashara wakubwa ili kuwatafutia soko la bidhaa zao wanazozizalisha na kuwawezesha kufikia viwango vya kuwa waekezaji na wafanyabiashara wakubwa.
Naye Meneja Mkuu wa Maendeleo kutoka Asasi Kilele ya Mazao ya Horticulture TAHA,Anthoy Chamanga katika maonesho hayo amesema pamoja na kuonesha teknolojia na mbinu mbalimbali za kilimo TAHA wamekuja na wadau wao ili kuhakikisha masuala yote ya mnyororo wa thamani ya mazao ya Horticulture kuanzia uzalishaji hafi sokoni yanapatiwa majibu.
Ameongeza kuwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu wameshiriki na kuonesha mbinu bora na teknolojia bora za kilimo pamoja na wasindikaji wadogo ambapo ameipongeza na kuishukuru serikali kwa kuendelea kuyafanya maonesho hayo mkoani Arusha na sehemu nyingine nchini kuwa ya mafanikio makubwa na kuwafkia wakulima wengi zaidi.
Vilevile amesema kuwa ni vyema wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali wakajikita katika kuyaboresha maonesho hayo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi kusudi waweze kufahamu faida ya muhudhuria maonesho hayo kwani teknolojia nyingine huwezi kuziona katika maonesho mengine huku akitolea mfano kilimo cha mazao ya horticulture kwa vitendo na kusema kuwa siyo sehemu nyingi katika maonesho kama hayo ukaenda na kuona teknolojia hizo.







0 Comments