Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mheshimiwa Abdallah Ulega amekabidhi madawati 250 kwaajili ya shule tatu za Kata ya Mwandege na Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga mkoani Pwani kwa lengo la kutimiza ahadi yake ya kumaliza kero ya upungufu wa madawati wilayani humo.
Akikabidhi madawati hayo kwaniaba ya Mbunge wa jimbo hilo Mheshimiwa Abdallah Ulega katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule za msingi Mwandege na shillingi ya Sekondari Lugwadu Katibu wa Mbunge Shein Kilindo amesema madawati hayo ni kwaajili ya shule za Sekondari za Lugwadu ya Kata ya Mwandege madawati 50, shule ya msingi Mwandege madawati 100 ya Kata ya Mwandege na Madawati 100 ya shule ya msingi Maliasili ya Kata ya Vikindu.
Kilindo amesema madawati hayo ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa jimbo hilo ambaye alitoa ahadi ya kuletwa Madawati hayo 250 kwaajili ya shule hizo tatu mwishoni mwa wiki akiwa kwenye Ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo jimboni humo ambapo alisema ili kumaliza kero ya upungufu wa madawati atatoa madawati hayo.
Amesema Mheshimiwa Ulega ameguswa na jambo hilo akiwa ni Mbunge wa jimbo hilo kwa Wananchi wake na leo ametimiza ahadi yake na ataendelea kuchangia mpaka changamoto za jimbo la Mkuranga zitakapokwisha.
"Mheshimiwa wetu hajamaliza kuchangia pale Mwenyezi Mungu atakavyomjaalia ataendelea kukabidhi madawati katika Shule zote za jimbo hilo la Mkuranga kwasababu ndio jimbo lake na eneo lake la kazi" amesema Kilindo.
Diwani wa Kata ya Mwandege Nassoro Nassoro akipokea madawati hayo amemshukuru Mheshimiwa Abdallah Ulega kwa imani aliyonayo kwa Wananchi wa jimbo hilo la Mkuranga kwa kutekeleza ahadi yake kwa shule hizo tatu.
Aidha amewataka Wananchi wa Kata ya Mwandege kuendelea kumpa ushirikiano Mbunge huyo ambaye anania ya Kweli kusaidia Wananchi wa jimbo hilo la Mkuranga kuwaletea Maendeleo.
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Mkuranga Jessey Mpangala baada ya kushuhudia makabidhiano ya madawati hayo amemshukuru Mheshimiwa Ulega kwa ziara anazofanya jimboni humo bila kuchoka ambapo alichukua changamoto alizokuta kwenye ziara yake na kufanyia kazi.
"Tumeona matunda ya ziara zake na Leo tunaona utekelezaji wake kwani madawati hayo yatasaidia sana kupunguza changamoto na haya madawati Wanafunzi wetu watayatumia"
"Na Sasa hivi watoto wetu wa darasa la Saba wanaelekea kwenye Mitihani ya darasa la Saba na tuna upungufu wa madawati ambapo Wanafunzi hukaa mmoja mmoja kwenye dawati moja watayatumia madawati hayo"






0 Comments