Header Ads Widget

TMDA YAONYA MATUMIZI YA DAWA AMBAZO HAZINA USAJILI NCHINI

 



Na Mwandishi wetu, Lindi


Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kusini imeonya matumizi holela ya dawa ambayo yamekuwa na madhara makubwa kwa afya hasa kwa kijana ndogo.


kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ngongo mkoani Lindi Mkaguzi wa Dawa  TMDA Kanda ya Kusini Elias Magambo  alisema baada ya kufanya mazoezi mbalimbali ya ukaguzi wakabaini uwepo wa matumizi ya dawa zilizoisha muda na zingine amabzo hazina usajili nchini.


Alisema kuwa katika maonyesho huwa wanatoa elimu  namna gani mwananchi anaweza kuangalia na kubaini kama dawa imesajilia ama la.


 “Huwa tunfanya mazoezi mbalimbali ya ukaguzi ukiwa na lengo la kulinda jamii inayotumia dawa vifaa tiba pamoja na vitendanishi na tumekuwa tukibaini makosa mbalimbali ambayo hufanywa na watoa huduma”


“Tumekuwa tukikutana na ukiukwaji wa sheria ya kutumia dawa ambazo zimeisha muda wake ambao kupitia maonyesho haya tumekuja kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kutumia dawa zilziosajiliwa na zinazotambuliwa na mamlaka hiyo”



“Wapo baadhi ya wanawake wengine ni watoto tena wamekuwa wakitumia sindano ili kuweza kuzuia ujauzito ambapo wazazi wamekuwa chanzo kikubwa cha watoto hao kupata ujauzito bila kujali maambukizi ya Ukimwi”


"Wapo wafanyabiashara wasio waadilifu wanauza dawa ambazo hazina Viwango Wala hazijasajiliwa nchini  na  huwauzia watu bila kujali  madhara yake ni makubwa kiasi gani na wataathirika vipi?



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI