Header Ads Widget

KAMPUNI YA ETG YATOA HUDUMA KWA ZAIDI YA WAKULIMA 10,000 KANDA YA KUSINI

 



Na Mwandishi wetu, Ngongo

Meneja wa Matawi ya ETG Inputs Ltd kanda ya kusini na Afisa Kilimo Kiongozi wa Kampuni hiyo, Victor Saimon amesema kuwa wamejipanga kutoa elimu kwa wakulima wote wa kanda ya kusini ili waweze kutumia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.


Akizungumza katika viwanja vya maonyesho ya kilimo vya ngongo alisema kazi yao kubwa ni kuuza na kusambaza mbolea, viwatilifu, mbegu za mbogamboga na mahindi pia kutoa mafunzo ya Kilimo (Agronomia).


“Sisi tunatamani kuona mkulima anakuwa kwakuwa kukua kwake ndio matarajio yetu ambayo yatatuwezesha na sisi kukua kikampuni na pia akipata matokeo chanya atakuwa mteja wetu wa kila siku”


“Tumeanza na vipando kwakutumia bidhaa zetu ili mkulima ajue matumizi sahihi ya viwatilifu na kuona namna bidhaa hizi zinafanyakazi ili wakulima waweze kulima kwa tija na mwitikio wa wakulima ni mkubwa hata matokeo yake ni makubwa na wamekuwa mashahidi na wameona ni bidhaa bora wako tayari kutuunga mkono”



“Zaidi ya wakulima 10,000 wamefikiwa wa mazao mbalimbali tukiwa na lengo la kuwaboresha kiuchumi ambapo mwaka huu tumeona idadi ya wakulima ni kubwa na pia tuna kitengo cha agronomy lengo ni kuwafikia wakulima moja kwa moja na hawawapatii wakulima namna gani ya kuvitumia ambapo wakitumia bila maelekezo wanaweza kutotumia kwa usahihi”


“Katika maonyesho haya tunatoa mafunzo kwa wakulima ambapo tumeandaa mashamba darasa ili kuwafundisha wakulima na pia tumekuja na bidhaa zetu” alisema Saimon



Daudi Panja Afisa Kilimo wa Kampuni ya ETG Inputs Ltd amesema wanayombolea ya kupandia na  kukuzia mazao na yakuzalishia mazao mbalimbali pomoja na mbolea za kupulizia ambayo hupulizia kwa mazao yote.


Ofisa kilimo ETG Inputs Ltd Amani Kansio  alisema kuwa wanazodawa za kila aina ambazo hutumiwa katika kuuza nyasi kwenye mazao yote pamoja na sumu za kuua wadudu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI