na Mwandishi wetu, Lindi
Mtafiti Mwandamizi wa zao la Muhogo kutoka Taasisi (TARI) Naliendele Bernadetha Kimata amewashauri wakulima wa zao la muhogo kutumia mbegu bora za zao hilo ili kuzalisha kwa tija.
Akizungumza katika viwanja maonyesho ya wakulima vya Ngongo vilivyopo Mkoani Lindi alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakigawana mbegu bila kuzingatia ubora hali ambayo imekuwa ikipelekea mihogo mingi kuwa na magonjwa.
“Unajua muhogo ni zao muhimu ni chakula kikuu huku kusni ukiangalia kiasi ambacho inazlisha ni wapili kwa nchi ambapot unazalisha asilimia 28 inayozalishwa nchini ambayo ni tani milioni8.2”
“Kipindi cha nyuma wengi walitumia mbegu za asili ambazo zilikuwa na changamoto na tija kuwa ndogo ambapo walikuwa wanapata tani 8 hekta moja pia hushambuliwa na magonjwa ya mihogo ambayo ni michirizi kahawia ambayo huathiri mti, majani na muhogo wenyewe’
“Wakati mwingine uzalishaji unakuwa wa chini ambapo husababsiha hasara kubwa kwa mkulima ambapo suluhisho ni matumizi ya mbegu bora za muhogo zaidi ya 13 ambazo zinatija ya hali ya juu ambapo ukitumia mbegu bora unapata tani 20-50 kwa hekta”
“Hii husaidia wakulima na vijana na wanawake ambao wakizalisha kwakutumia mbegu hizo hazipati magonjwa hivyo kuhimili tuko katika hatua nzuri ya kuweza kumsaidia mkulima ambapo atazalisha na kuuza kwa usalama”
"Kitendo cha kugawana mbegu za muhogo kulikuwa kunaongeza magonjwa katika mihogo lakini leo mzalisjaji anaweza kualisha mbegu zake akalima na baade akauza kwingine”






0 Comments