Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima APP Dodoma
MKURUNGEZI Mkuu wa Tume ya TEHAMA ,Dkt Nkundwe Mwasaga amesemaTEHAMA imesaidia masuala mbalimbali hapa nchini ikiwemo huduma za fedha kupitia benki.
Hayo ameyasema leo jini hapa na Mkurungezi huyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa TUME hiyo na Muelekeo wake Katika Mwaka wa Fedha 2023/24.
Mkurungezi huyo amesema kuwa kwa sasa mwananchi anaweza kufanya shughuli za kibenki bila ya kujiangaisha kufika benki .
"Tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika TEHAMA kwani hapa nchini kampuni mbalimbali zimetengeneza mitaji mikubwa na zinafanya kazi nchi nyingi duniani,"
Na kuongeza"Hadi sasa TUME imeshasajili wataalam wa TEHAMA 1,600 wanaohudumia nchi nzima," Amesema Mkurungezi huyo Mwasaga
MAFANIKIO YA TUME KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2022/2023
Nipamoja na Kuanzishwa kwa mradi wa kujengwa kituo kikubwa cha Taifa cha Ubunifu Dar Es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma kwa wataalam, watafiti, na wabunifu wa TEHAMA.
Kuanzisha kituo kimoja cha ubunifu TEHAMA (Softcentre) Zanzibar, vinne vya Kanda katika majiji ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Lindi na Mbeya kwa ajili ya kuendeleza kampuni changa za TEHAMA na kuendeleza kituo cha Dar es Salaam ili kukuza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa za TEHAMA na kukuza uchumi wa nchi.
Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT refurbishment and assembly centre).
Kuwezesha mafunzo maalum ya TEHAMA kwa wataalam kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.
"lengo la mfumo huu ni kutambua bunifu na kupanua wigo wa ukuzaji wa wabunifu na bidhaa na huduma za TEHAMA zinazozalishwa Tanzania na hivyo kukuza pato la Taifa na kuongeza fursa za ajira kupitia TEHAMA na maendeleo ya kidijitali duniani," Amesema.
VIPAUMBELE VYA TUME KWA MWAKA 2023/2024*
Kuendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar.
Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly centre).
Kuwezesha uanzishaji wa vituo vya majaribio vya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation hubs) katika Wilaya 10.
Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya TEHAMA.
Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa Amesema Serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya Kidijitali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo msimamizi mkuu unafanywa na Tume ya TEHAMA.
" Hili ni jambo kubwa kwani fedha nyingi imewekezwa kwa ajili ya kuboresha TEHAMA nchini kwani shughuli mbalimbali kwa sasa duniani zinafanyika kwa njia ya kidijitali ikiwemo huduma za malipo mabalimbali, huduma za afya za matibabu, uzalishaji, kilimo, uchimbaji wa madini," Amesema Msigwa.
Hata hivyo Majukuu makuu ya Tume ya TEHAMA ni kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya TEHAMA, katika Sekta zote binafsi na Taasisi za Serikali, Kukuza TEHAMA kwa kuwawezesha wataalam wenye uwezo katika kufanya shughuli zote zinazohusu TEHAMA nchini, pia kuifanya Tanzania kushindana kidunia katika utekelezaji shughuli za TEHAMA.
0 Comments