Header Ads Widget

MBARONI KWA KUMCHOMA MTOTO WAKE KWA MAJI YA MOTO

 


NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA .


Mwanaume mmoja ajulikanae Kwa jina la Maneno Thomas mwenye umri wa miaka 35 Mkazi wa Chamagati Wilaya ya Sengerema Mkaoni Mwanza anashikiliwa na jeshi la polisi Kwa tuhuma za kumchoma mikono Mtoto wake Kwa maji ya moto. 


Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani hapa Wilbroad Mtafungwa ameeleza kuwa mtuhumiwa huyu alitenda kosa Hilo mnamo tarehe 30 julai mwaka huu muda wa saa mbili usiku baada ya kutoka katika shughuli zake.


Mtafungwa ameeleza kuwa mtuhumiwa huyu alimwambia Binti yake aitwaye Prisca Maneno mwenye umri wa miaka 11apike chakula Cha usiku ndipo alipoelezwa kuwa hakuna mboga kwani ililiwa na mdogo wake Daniel Mwenye umri wa miaka 9.


"Maneno Thomas alishatengana na mkewe  kutokana na vitendo vyake vya kipigo Cha mara Kwa mara na mwanamke aliamua kuondoka" Alisema Mtafungwa.


Amesema kuwa mtuhumiwa aliwasha moto kisha kuchemsha maji yalipochemka alimuita mwanae aitwaye Daniel Maneno na kumwagia maji hayo katika mikono yake yote miwili na kumsababishia maumivu makali.


Baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa aliamua kumfungia Mtoto huyo chumbani kwake na wananchi wa eneo hilo washtuka kutokumuona Mtoto Daniel siku mbili mfululizo ndipo walipoanza kufatilia na kugundua amefanyiwa ukatili huo.


"Haikuwa kawaida ya Mtoto huyo kutoonekana wakaanza kufatilia walupokiridhisha walimuzuia mtuhumiwa chini ya ulinzi bila kujichukulia sheria mkononi na kumfikisha kituo Cha polisi" Alisema Mtafungwa.


Aidha Amesema kuwa mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo la kikatili Kwa mtoto wake baada ya kupata hasira kuwa mwanae kula mboga yote.


Hata hivyo ametoa wito Kwa wananchi kuendelea kuripoti na kifichua vitendo vya kikatili vinavyoendele kutendeka katika jamii, na  mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI