Header Ads Widget

SERIKALI YAENDELEZA JITIHADA ZA KUREJESHA MBWA MWITU, SERENGETI

 



Na,Jusline Marco; Arusha


Serikali kupitia Taasisi zake TAWIRI na TANAPA imeendelea  na zoezi endelevu la kuwarejesha mbwa mwitu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni kuhakikisha mbwa mwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo ikolojia ya Serengeti.



Akizungumza wakati wa zoezi la kuwapokea mbwa mwitu wapatao 20  waliozaliwa Hifadhi ya Taifa Mkomazi na kuletwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kabla ya kuachiwa huru, Dkt. Emmanuel Masenga ambaye ni Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti Serengeti amesema kuwa matokeo ya tafiti yanaonyesha kuwa sababu kuu za kutoweka kwa mbwa mwitu katika hifadhi ya Serengeti ni magonjwa (Rabies and Canine Distemper Virus) na ongezeko la idadi ya simba na fisi pamoja na kuuwawa na wananchi wanapotoka nje ya hifadhi.



Aidha Dkt. Masenga  amesema jitihada za Serikali  za kuwarejesha mbwa mwitu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ni zoezi endelevu na lilianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kuhifadhi mbwa mwitu kwa ajili ya kutunza bioanuwai na kuendeleza utalii.



Dkt. Masenga  amesema kama inavyofahamika jukumu kubwa la Taasisi  ya  Utafiti  Wanyamapori  Tanzania (TAWIRI) ni kufanya  tafiti  za wanyamapori, hivyo TAWIRI  inaendelea kufanya tafiti za kina za kuhakikisha kuwa mbwa mwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo ikolojia wa Serengeti.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI