Header Ads Widget

FISI KUIBUKA KWENYE TAMASHA LA UTAMADUNI NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE.


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa Amewaomba wananchi kuhudhuria Tamasha la Utamaduni ambalo linafanyika Kwa Mara ya Kwanza Mkoani Njombe na Ikiwa ni Mara ya Pili tangua Kuanzishwa Kwake  ambapo tamaduni za makabila yote ya mikoa ya Tanzania zitaonyeshwa Huku Mkoa wa Njombe wakiwa wenyeji.


Akizungumza Katika Viwanja vya stendi ya zamani mjini  Njombe ambako tukio  hilo lItafanyika kwa takribni siku nne Mkuu huyo wa  Wilaya Kasongwa  ametoa wito Kwa Wananchi Kujitokeza Ili Kujionea mambo ya Utamaduni  unavyo Dumishwa na Watanzania Hapa Mkoani Njombe.


Kasongwa amesema katika tamasha Hilo atakuwepo mnyama Fisi ambaye atakuwa akitembezwa katika eneo la uwanja wa stendi ya zamani ambako Tamasha litafanyika.



Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Eliudi Mgeni Anasema Ujio wa Tamasha la utamaduni hapa mkoani Niombe unaenda kuleta mageuzi makubwa ya kibiashara  kwa wananchi  na wafanya biashara wenyewe.


Nao Badhi ya Wananchi  Waliozungumza na kituo Hiki wamewataka Wananchi Kutoka Mkoa Huu Kuchangamkia Fursa ya kujitokeza ili wajionee namna utamaduni wa mtanzania unavyo oneshwa kwa mara ya kwanza njombe.



Tamasha la Utamaduni  ambalo linatarajiwa kuzinduliwa hapo kesho na waziri wa sanaa michezo na utamaduni Balozi Pindi Chana  litajumuisha wageni kutoka makabila  yote ya mikoa ya Tanzania  huku likifanyika kwa mara ya pili tangu kuanzishwa kwake hapo mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI