Ndiye mkuu na mmiliki wa kikundi cha Kirusi cha makampuni "Concord", mwanzilishi wa PVK Wagner. Anachukuliwa kuwa mmoja wa marafiki wa Rais wa Urusi Vladimir Putin . Shujaa wa Shirikisho la Urusi , shujaa wa DPR na shujaa wa LNR .
Anaongoza Kundi la Wagner, muundo wa kijeshi unaoungwa mkono na serikali ya Urusi na kushiriki katika migogoro ya kijeshi barani Afrika, Syria, Ukraine na maeneo mengine ya ulimwengu.
Kampuni "Concord" ilijishughulisha na upishi wa maafisa wa hali ya juu zaidi nchini Urusi, shukrani ambayo iliitwa "mpishi wa Putin" kwenye vyombo vya habari.
Mnamo 2016, alijumuishwa katika orodha ya watu 30 mashuhuri zaidi wa Saint Petersburg kulingana na chapisho la Gorod 812.
Tangu 2016 imekuwa chini ya vikwazo vya Marekani , tangu 2020 chini ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya na Uingereza, tangu 2022 Australia, Canada, New Zealand na Japan .
Mnamo Julai 2022, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza zawadi ya dola milioni 10 kwa taarifa kuhusu Prigogine na wafanyakazi wengine 12 wa Wakala wa Utafiti wa Mtandao kuhusiana na madai ya kuingiliwa kwa michakato ya kisiasa na uchaguzi nchini Marekani. FBI imetoa zawadi ya hadi $250,000 kwa usaidizi wa kumkamata.
Kundi la Wagner liliibuka kidedea zaidi katika vita vya kuwania mji wa Bahmut mwaka wa 2022 na 2023.
Alianzisha uasi wa muda mfupi wa kutumia silaha dhidi ya Vikosi vya Wanajeshi vya Shirikisho la Urusi na Wizara ya Ulinzi mnamo Juni 23, 2023
-Amuawa kwenye ajali ya ndege
-Alianza kama mwizi wa hereni kwa ukabaji, akaja kuwa mpishi wa Putin, na mwisho ‘ Chinjachinja’.
-Hajawahi hata kupitia mafunzo ya mgambo, ajabu anaongoza jeshi la watu 25,000.
Anaitwa Yevgeny Viktorovich Prigozhin. Alizaliwa mwaka 1961. Ni kwenye mji mmoja na Vladimir Putin. Mji wa Leningrad (Sasa Saint Petersburg).
Wawili hawa; Putin na Prigonizj ni marafiki. Wote ni ‘Watoto wa Mjini’. Wametokea kwenye maisha ya familia za kimasikini.
Tofauti yao kubwa moja ni kuwa, Putin amejiongeza kwenye shule yake. Akapitia jeshi na mafunzo ya ukachero kwa viwango vya KGB.
Putin ni jasusi mbobevu na mwenye hulka ya kumtilia mashaka yeyote yule, hata mbwa wake.
Prigonizj ana uzoefu wa kijelajela. Miaka ya 80 mwanzoni akiwa ametoka kulewa na vijana wenzake mjini Leningrad, Prigonizj, na kwenye usiku wa maneno, alimwona mwanamke anapita barabarani amevaa viatu vizuri na cheni ya dhahabu shingoni.
Prigonizj akawashawishi wenzake wamsemeshe mwanamke yule. Hapo hapo Prigojizj akamrukia kwa kabali na kumvua cheni na viatu. Mwanamke yule alizimia. Prigonizj alihukumiwa miaka 13 jela.
Alipotoka jela miaka ya 90 Prigonizj akaikuta Soviet Union ( Urusi ya zamani) iliyosambaratika. Kwenye Urusi mpya Prigonizj alianza kujituma kwa kukaanga na kuuza soseji nje ya moja ya maduka makubwa.
Prigonizj ni mbunifu kwenye biashara. Akaendelea mpaka akapata mtaji wa kuanzisha duka la mvinyo, na baadae akaanzisha mgahawa wa kisasa ulioitwa ‘ The New Island’.
Wakati huo Putin alikuwa Meya wa Jiji Msaidizi. Putin akawa mtembeleaji, ama mteja mkubwa wa Prigonizj.
Ndipo hapo wawili hawa wakafahamiana na kuwa marafiki.
Putin alipohamia Moscow na kuingia Ikulu ya Kreml, na kwa hulka yake ya kijasusi ya kuwatilia mashaka watu, alianza kuwavuta Ikulu watu aliowafahamu tangu akiwa Leningrad. Mmojawapo akawa Prigonizj.
Tangu hapo, Prigonizj akaanza kupewa tenda kubwa kubwa za kusambaza vyakula. Utajiri na umaarufu wa Prigonizj ukaongezeka.
Kwanini marafiki hawa wamefikia kugombana?


.jpg)

.jpg.webp)




0 Comments